Tatizo Sio Raslimali Zilizopotea


TATIZO HUTAKI KUAMUKA MAPEMA.
katika kitabu changu cha kwanza cha kutoka sifuri mpaka kileleni nalikushirikisha kwamba kulala mapema na kuamka mapema, kunakufanya kuwa mtu mwenye afya njema sana, tajiri na mwenye busara.

Moja kati ya imani ambazo vijana wengi wanazo ni imani kwamba kuna mambo ambayo wao hawapaswi kufanya hivyo yanafaa yafanywe na wazee. Mfano kuna MTU nilimwambia kwamba naandika kitabu basi akawa ameniambia kwamba vitabu wanaandika wazee ambao wanakuwa wamezeeka wanawashirikisha watu safari nzima ya maisha yao. Lakini mimi nilimjibu kwamba nataka nipate akili ya uzee nikiwa bado kijana. Na hili ndilo najitahidi kufanya na kuhakikisha kwamba napata kila siku. Kama kuna vitu wanapaswa kuwa navyo wazee tu lakini Mimi naweza kufanya kazi kuhakikisha kwamba nimevipata, basi nitafanya kazi kuhakikisha kwamba nimeviapata ili  nione nitakosa nini kama nitavipata nukiwa bado kijana!! Au nione kitu gani kitapotea nikishapata vitu hivyo!

Moja kati ya vitu hivyo ni hivyo vitatu ambavyo vinaelezwa na msemo huo hapo juu

msemo unaosema kwamba kulala mapema na kuamka mapema kunakufanya kuwa mwenye afya njema sana, tajiri na busara.

Kama afya njema imewekwa kwa ajili ya wazee basi mimi nataka niwe nayo nikiwa bado kijana. Kama  utajiri ni kwa ajili ya wazee basi mimi nitakuwa nao nikiwa bado kijana.

Kulala mapema na kuamka mapema kunakufanya mwenye busara mwenye afya njema, na tajiri. Kuna siri kubwa sana katika kuamka mapema, kuamka mapema kunakufanya uweze kuitafakari siku yako,  uianze siku kwa kusoma Malengo Yako.

Ninapozungumzia kuamka asubuhi na mapema nunakuwa haswa nazungumzia saa 11 au saa 10 ,, watu wengi wanaona kama haiwezekani kuamka mapema lakini kuna vitu ambavyo vitakufanya uweze kuamka mapema.

1. Kuwa na sababu.
Kama una msukumo mkubwa sana ambao unakusukuma wewe kutimiza Malengo Yako ya maisha basi hutalala, mpaka pale utakapokuwa umetimiza malengo yako. Ukilala kitakachokuja akilini mwako ni malengo yako.  Kumbe kama hauna Malengo mpaka sasa hakikisha kwamba unaweka mpango mkubwa sana leo, utakaokufanya uendelee kuyafikiria Malengo Yako hata kama umelala. Malengo ni nguvu au moto ambao ukiuwasha haupaswi kuzimika mpaka pale utakapokuwa umeyatimiza.
2.  Weka alarm
Maisha siku hizi ni rahisi sana. Alarm itakuamusha muda wako ambao umeiambia. Ikipiga utahitaji kuamka muda huo hata kama hunisikii kufanya hivyo. Utagundua kwamba ukishaamuka afya yako itakuwa vizuri na utaendelea vizuri na ratiba Yako. Utakuwa umeshinda vishawishi vilivyokuwa vinakuvuta kuedelea kubaki kitandani.
Kumbuka kwamba wakati unaanzisha tabia hii ya kuamka mapema utahitaji kutumia nguvu kubwa sana, kama ulivyo ukweli kwamba wakati ndege inaanzisha safari yake inatumia mafuta mengi sana kuliko ilivyo safari nyingine iliyobaki. 
Hivyo na wewe utahitaji kuweka juhudi kubwa sana wakati wa kuanzisha tabia hizi mpya. Weka nguvu mpaka pale tabia hii itakapomuwa imekuwa sehemu ya maisha Yako. Yaani kama ambavyo huwa unapiga mswaki bila kuuliza, basi ifikie hatua na wewe uanze kuamka asubuhi bila kuuliza.
Tukutane kileleni..
MUHIMU SANA;
Kuna semina ya ambavyo nimeipa kichwa cha TIMIZA MALENGO YA MWAKA MZIMA NDANI YA MIEZI SITA.  Ndio namaanisha miezi sita. Ndani ya semina utapata kujifunza mambo mengi sana yatakayokusaidia sana wewe kutimiza malengo yako mwaka huu. Kikubwa zaidi katika kutekeleza na kutimiza malengo yako nimekuja na mfumo Mpya ambao binafsi nimeutumia ndani ya miezi sita na umenipa matokeo makubwa sana katika kutimiza malengo yangu. Mfumo huu unaitwa MFUMO WA NYUMBA (HOUSE SYSTEM). Huu ni mfumo Mpya hapa duniani, na binafsi nimeutumia umenipa matokeo makubwa. Naenda kuwa nakudadafulia mfumo huu kwa undani kwenye semina hii ambayo nitaiendesha. Kiufupi kosa mengine mwaka huu ila usikose kujifunza mfumo huu ambao unaitwa MFUMO WA NYUMBA.

Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao kupitia katika kundi la waspu la HAZINA.
Hii ni kutokana na hali ya kwamba

1. mtu yeyote anaweza kuhudhuria semina hii akiwa hata nyumbani kwake bila kutumia gharama nyingi za usafiri kuja huku nilipo Mimi.

2. Lakini pia kutokana na ukweli kwamba mtu yeyote yule ambaye Yupo kwenye kona yoyote ile ya dunia anaweza kuhudhuria semina hii.

3. Gharama za uendeshaji wa semina zinapungua hivyo kukuwezesha wewe kuweza kuhudhuria semina bila kikwazo chochote kile.

JINSI YA KUJIUNGA NA SEMINA HII.
Gharama ya semina hii ni kiasi kidogo sana cha 20,000/- za kitanzania. Hii ni gharama ndogo sana kulinganisha na kitu kikubwa sana ambacho unaenda kukipata ndani ya semina hii itakayoanza mwezi wa saba tarehe 15 mpaka tarehe 19.

Jinsi ya kulipia.

Tuma pesa kupitia namba ya voda MPESA 0755848391 yenye jina la GODIUS RWEYONGEZA. baada ya hapo nitumie ujumbe wenye neno HAZINA wasapu namba 0755848391. Ili niweze kukuunganisha kwenye mundi hilo tayari kwa ajili ya semina hii.

MANUFAA MENGINE YA KUNDI LA HAZINA.
1. Kwanza kabisa ni muhimu sana kufahamu kwamba kundi la hazina ni  tofauti na makundi mengine ya wasapu ambayo umeyazoea. Kundi hili lina watu makini ambao wapo tayari kuhakikisha kwamba wanatimiza malengo yao. Watu walio katika kundi hili huwa wanalipia elfu ishirini kila baada ya miezi sita kuwa katika kundi hilo.

2. Lakini pia kuwa katika kundi hili kutakuleta karibu sana na Mimi ambapo nitakuwa tayari kukusaidia na kuongea na wewe hapo muda wowote ule kuhakikisha kwamba unafikia Kile kilichobora zaidi.

3. Lakini pia nitahakikisha kwamba tunafanya kazi bega kwa bega ili kuhakikisha kwamba unatimiza Malengo yako ndani ya miezi sita.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa sasa siwezi kuwa kwenye kila kundi na kumsaidia kila mtu maana ninazo kazi nyingi sana ambazo zimenibana, hivyo kuwa kwako katika kundi la hazina ni kitu ambacho kitatufanya tuwe karibu sana muda wote.

4. Lakini pia utapata nafasi nzuri sana ya kuhudhuria semina ya kufungua mwaka 2018 bure kabisa. Hii ni kutokana na ukweli kwamba bado ada yako ya miezi sita itakuwa bado haijaisha hivyo utazidi kupata kilichobora sana kutoka kwangu.

Hivyo hakikisha kwamba haukosi nafasi hii adimu sana kwako kuweza kufanya mambo makubwa sana.

Hakikisha hauikosi nafasi hii adimu
Ni Mimi Rafiki na ndugu yako
Kocha Godius Rweyongeza
0755848391
godiusrweyongeza


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X