HAYA NDIO MAMBO MAWILI AMBAYO UNAHITAJI KUYAZIKA.
Habari za siku ya leo rafiki na ndugu msomaji wa makala za songa mbele. Imani yako leo ni siku njema sana na kila kitu kinaenda vizuri kama umenga. Ni jambo jema sana kwamba leo tunaenda kujifnza  kitu kipya na cha tofauti kitkachotutoa sehemu moja kwenda sehemu nyingine katika maisha yetu.
Katika maisha kuna baadhi ya vitu ambavyo vimetuzunguka na vipo katika mazingira yetu ambavyo huwa vinatururudisha nyuma. Viitu vipo kwenye mazingira na mara nyingi ni kwamba wanaovikumbatia vitu hivi kuendelea kuwepo ni wewe. Vitu hivi vinakurudisha nyuma na kukufanya uzidi kuishi maisha ambayo ni ya kawaida. Unaridhika wakati hujaweza kaupata kile ambacho unakihiytaji.  Vitu hivi tunaweza kuviita adui mkubwa wa mafanikio yako.
Adui huyu kiukweli hayupo mbali sana na pale ambapo wewe upo. Adui  hawa wapo karibu sana na wewe na kitu kikubwa unachopaswa kufanya sasa hivi na kuhakikisha kwamba unawachungulia na kuwaangalia. Umesikia wakisema kwamba adui yako unapaswa kumpenda. Hii ni kweli kabisa. Lakini katika makala hii tunaenda kujifunza jinsi ya kumpenda zaidi adui wetu huyu, hatimaye tumzike yeye. Endapo adui huyu hutamwondoa kwenye mlolongo wa maisha yako basi watazidi kukuvuta na kukurudisha chini. Kumbe ni muhimu sana kuhakikisha kwamba adui huyu unamfukuzia mbali kwa maana adui huyu hana manufaa makubwa sana kwako.
1.      UOGA
Uoga ni adui na,b ari moja wa mafanikio mengi sana. uoga sio kitu kikubwa sana ya ya ile hofu ambayo mtu anaijenga ndani yake. Uoga unawazuia watu wengi sana kuendelea na kazi zao. Kikubwa sana kuhusiana na uoga ni kwamba uoga unawazuia watu wengi sana kuchukua hatua kubwa na kuishi maisha ambayo kila mtu ameletwa hapa duniani kuyaishi. Dunia ni sehemu njema sana ya kuishi kama utaishi kusudi lako na kuhakikisha kwama unafanya kile ambacho unapaswa kuwa unafanya kwa wakati husika. Muda wa kuanza kuogopa kwanza utakuja kuishi siku nyingine kwa sasa haupo tena.
Hakikisha kwamba unaondokana na uoga wa aina yoyote ile. Anza kuishi kwa namna ya tofauti. Fanya kazi kwa namna ya tofauti. Ondokana na uoga, itumie sana akili yako maana akili yako ndicho chombo pekee ambacho  umejaliwa na mwenyezi mungu chenye uwezo kubwa san akauliko kompyuta au mashine kubwa yoyote ile ambayo imewahi kutunehgenezwa katika ddunia hii.
2.      UMENEJA.
Kuna kazi kubwa sna ambayo unaifanya kwa sasa. Kwanza nikupe hongera kwa sababu tu kwamba kkuna kazi ambayo unaifanya. Hivi una uhakika kazi hii unayoifanya inakulipa hata kidogo? Hivi kazi hii ambayo unaifanya inakuongezea thamani gani? Mbona unapoteza muda mwingi sana kufanya kazi ambayo haiongezi tahamni kwenye  maisha yako? ndio, hii ni kweli kabisa. Upo unafanya kazi hii  na unapoteza muda mwingi sana kufanya kazi ambayo hata haikufai wala haitkja kukusogeza mbele katika maisha yako. naam, hii ni kazi ya kutafuta umbea.  Hii ni kazi ya umeneja wa g=duni aambayo bumejipa mwenyewe ingawa una uhakika kwa asilimia 100 kwamba haikulipi na inakupotezea muda wako.
Umbea haulipi. Hailipi pia kuwa mtandaoni muda wpte ili kutafuta nani kamposti nani? Na nani anafanya nini? Hailipi pia wewe kukaa mtandaoni na kuanza kuweka picha kila wakati. Kuwa makini. Watu makini wana uchungu na muda waoo na wanahakikisha kwamba wanautumia muda wao katika kuhakikisha kwamba wanatoka hapo walipo na kwenda hatua ya ziada. Binadamu ni mtu ambaye anapaswa kukua kila siku katika utendaji wake wa kazi. endapo utaona kwamba haujafanya vitu  kwa namna ya tofauti siku ya leo, jua kwamba kuna vitu vikkubwa sana unapoteza. Huu ndiomuda wako kuhakikisha kwamba unawekeza nguvu kubwa sna katika kuutumia muda wako vizuri sana.
Utumie muda wako kuhakiksha kwamba unajifunza kitu kipya kila siku kkaktika maisha yako. muda ni mali. Kama utaupoteza leo katika kufanya vitu amabvyo hata haavina manufaa kwako basi utakuwa unajiua wewe mwenyewe. Ili kuweza kuepuka kujiua mwenyewe, basi naomba  uzike tabia hizi mbili ambzo tumeziona kwa siku ya leo ili uweze kuzidi kusonga ,mbele.
Ni mimi rafiki yako na ndugu yako.
KOCHA GODIUS RWEYONGEZA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X