Hivi Ndivyo Unaweza Kuwanasa Watanzania Wengi Kwenye Mtego Mmoja


.

Habari za siku hii ya leo Rafiki na ndugu msomaji wa blogu Yako ya songambele. Imani yangu leo ni siku njema sana, na unaenda kufanya mambo makubwa sana. Jiambie kwamba hata iweje lazima leo nitoboe. Lazima leo nifanye mambo kwa namna ya tofauti sana.

Kisha baada ya hapo nenda kazini kapige kazi. Kumbuka kwamba siku zinazidi kusogea na mwaka unakaribia mwishoni, hivyo endelea kuweka juhudi kubwa sana ili uweze kuyakamilisha malengo yako ya mwaka huu.

Karibu sana tuendelee na makala yetu ya leo.

Watanzania wengi ni watu ambao wanapenda sana mafanikio ya haraka. Watanzania ni watu ambao hawapendi kujishughulisha na kazi ngumu sana ila wanapenda mafanikoo makubwa sana. Hii ni kwa mujibu wa utafiti Wangu mdogo ambao nimeufanya siku za hivi karibuni.

Hivyo kutokana na watanzania kutokupenda kujihangaisha wamejikuta wakipenda sana kazi zile ambazo ni rahisi sana kufanyika, wamejikuta wakipenda kuambiwa kwamba unaweza kufanya kazi fulani leo kesho asubuhi ukaibuka ukiwa tajiri mkubwa sana. Huu ndio ukweli na hizi ndizo habari wanazopenda watanzania.

Kumbe kama kuna mtego ambao mtu anaweza kuutega, basi ni mtego wa kuwaambia watu kwamba Nina kazi au dili ambalo linaweza kukulipa ndani ya wiki moja tu ukawa milionea. Hapo MTU atalazimika kuuza kila kitu kinachomuhusu yeye ili asije akapitwa na mamilioni ya pesa hayo. Na Mara nyingi matapeli wamekuwa wakiutumia huu mwanya kuja na fursa nyingi sana kila siku. Kiasi kwamba watu wanahamasika sana na kujiunga na kazi au shughuli hiyo ambayo inaonekana kwamba inawaigizia kipato kikubwa sana kwa haraka sana.
Kila mtu atamwabia mwenzake, na cha ajabu hakuna hata mmoja anayehoji na kujiuliza inawezekanaje? Baada siku chache sana utakuta umewapata watu wengi sana kwenye mtego huo. Huu ndio ukweli unaowahusu watanzania.

Kwa upande mwingine ukitaka watu wakuchukie, wauchukie mradi wako waukumbikie, watu wakucheke. Basi waambie njooni tuwekeze kwenye mradi huu, tutakuja kupata mavuno baada ya miaka 10 au 20. Hapo mtatafutana, watu watakuona kama umechanganyikiwa na haujielewi kabisa.

Mfano, ukiwaambia watu kwamba tuwekeze kwenye miti, nunua shamba kwa hela kidogo mfano kwa Bukoba na Morogoro mikoa ambayo nimeizoea katika uuzaji na ununuaji wa mashamba unaweza kununua shamba la kuwekeza kwa  pesa za  zisizozidi hekali  kwa shilingi laki tano kwa hekari. Ingawa inaweza kuwa chini zaidi ya hapo au juu zaidi ya hapo kulingana na eneo katika mikoa hiyo tajwa.

Baada ya kununua ukaweka gharama za ununuaji na upandaji wa miti. Kitu ambacho kiujumla kinaweza kukuchukua laki tano nyingine. Jumla millioni moja, lakini baada ya hapo unakuwa na miti ni ya kwako na ardhi ni ya kwako.
Baada ya miaka isiyopungua kumi unakuwa tayari unayaona mamilioni ya shilingi mkononi mwako maana hayana namna ya kukuwepa.

Ukimwambia mtanzania hivi atacheka sana kisha ataondoka zake.

Sijui wewe baada ya kusoma hapo umekuwa na mwitikio gani. Lakini kitu cha msingi sana ni kwamba hakikisha kwamba unachukua hatua siku hii ya leo ili kuanza kufanya uwekezaji wa muda mrefu wala sio kupenda uwekezaji wa muda mfupi (ambao Mara nyingi sana unaambatana na utapeli), ukitaka  leo uweke shilingi elfu kumi na kesho upate mamilioni ya shilingi basi jua kwamba utapotezwa sana.

Kama kweli utakuwa tayari kuwekeza katika mradi huo ambao leo hii unawekeza elfu kuni au ishirini na kesho inaibuka na mamilioni ya shilingi basi hakikisha kwamba unakuwa makini na unafanya utagiti wa halo ya juu sana na kujiridhisha juu ya Kile ambacho unataka kufanyia uwekezaji.

Lakini pia tayari kufanya kitu ambacho una uhakika hakitakulipa leo wala hata kesho. Ila kikianza kuingiza mamilioni basi yatakuwa yakifuatana.

Soma vizuri makala hii maana imeweka vizuri tatizo na hatua za kuchukua katika lugha ambayo ni  kisanaa zaidi. Chukua hatua baada ya kusoma makala hii usikae na kusema kwamba nitafanya kesho au keshokutwa, maana muda wako wa kufanya kazi na kuhakikisha kwamba unakuwa Huru kiuchumi ni leo hii.

Usisahau kuwashirikisha watu wengine makala hii ili nao wazidi kupata Maarifa bora kama haya.

Jiunge pia na mfumo wetu wa upokeaji wa makala maalumu kwa watu maalumu kama wewe hapo kwa KUBONYEZA HAPA

Na 
Godius Rweyongeza
0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com
Asante


One response to “Hivi Ndivyo Unaweza Kuwanasa Watanzania Wengi Kwenye Mtego Mmoja”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X