Hivi Ndivyo Watu Wanapaswa Kuhukumiwa.


Habari za siku hii ya leo rafiki yangu imani yangu siku Yako ni njema sana. Hakikisha kwamba leo unaitumia vizuri sana maana leo hii ndio siku pekee kwako.

Katika maisha ya siku hizi kuhukumu watu ni jambo la kawaida sana. MTU akikuona unafanya kitu fulani basi kitu kikubwa sana ambacho anafanya, anakimbilia kukuhukumu na kutoa hoja zake. Kwa hakika mwanadamu hawezi kukosa cha kusema juu Yako. Hivyo ni muhimu sana kuhakikisha kwamba humezwi na hukumu ambazo watu wanatoa. Hukumu hizi zinawwza kukurudisha nyuma na kukuyumbisha sana.

Les Brown aliwahi kuandika kwamba “mtu 1 akikwambia huwezi, wanahitajika 17 kukwambia kwamba unaweza”. Kumbe usikubali mtu akwambie huwezi.

Najua  katika maisha Yako iwe kwa hiari au kwa kulazimisha ila umewahi kuhukumu. Linapokuja suala la kuhukumu wati wamekuwa wanahumukumu kwa hisia wala sio kwa kujihoji na kuuangalia uko wapi?

Lakini pia ni muhinu kufahamu kwamba usitake tu kukwepa kuhukumiwa. Wewe kama mwanamafanikio unapaswa kuwa MTU wa kusababisha matokeo na sio unasubiri vitu vitokee ili ufanye, Bali sababisha vitu vitukee na waache watu wakuhukumu, huku wewe ukiendelea na kazi yako.

Linapokuja suala la kuhukumu, Fanya hivyo au acha kabisa, ila hapa nakuomba unapohukumu usiangukie upande mmoja na kuuacha upande  wa mwingi e.

Mhukumu tu huyu kwa kuangalia malengo yake ya mbeleni basi! Hiki ni kigezo kikubwa ambacho kinaweza kumhukum tu!

Wala sio rangi yake, umri wake au kabila lake. Malengo ndiyo kitu ambacho unaweza kukitumia.
Je, ana mpago gani baada ya miaka mitano,
Je anafanya nini chenye thamnai kubwa sana? Hii ndiyo njia nzuri sana ya kumhukumu.

Ni muhimu oia kutambua kwamba siku zote unavuna  kile ambacho umepanda. Kama utahujumu, lazima utegemee kuja kuhukumiwa.

Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha kutoka songa mbele blog
Na
Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391

Kupata makala maarumu kutoka SONGA MBELE, bonyeza hapa na ujaze fomu.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X