Huu Ndio Wakati wako Kufanya Mabadiliko


kila kitu kina wakati wake.
Kuna wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna.
Wakati wa kubomoa wakati wa kujenga

(Mhubiri 3:3-8)

Kumbe kila wakati tunapofanya kitu kipya tunakuwa tunapiga hatua kutoka sifuri kwenda moja. ( From zero to one).

Kila unapoazisha kitu kipya umebadilisha mambo kutoka sifuri kwenda moja.

Kutokana na mabadiliko haya yanayotokea kila siku hatutegemei urudie kitu kile kile afu tuseme umeweza kutoka sifuri mpaka moja.

Solomoni alikuwa tajiri mkubwa kipindi chake lakini hakuwahi kugundua operating system. Wala hakuwahi kusikia habari za intanenti.

Vivyo hivyo wewe usianze kuiga na kufanya kile ambacho kila mtu anafanya.

Hatutegemei kwamba Billgate anayekuja atakuwa  amegundua operating system.
Mark Zuckerberg anayefuata sio kwamba atagundua FACEBOOK.
Diamond anayefuata sio kwamba ataimba BONGO FLAVA
Samata anayefuata sio kwamba ATACHEZEA TP MAZEMBE na kwenda ULAYA.
Eric Shigongo anayefuata sio kwamba atakuwa mmliki wa GLOBAL PUBLISHERS.

Kama unawaiga hawa watu.
Na kufanya kama wanavyofanya. Basi sina uhakika kama una lengo LA kutoka sifuri mpaka moja.( From Zero To One)

JITOFAUTUSHE MWENYEWE AU KUFA ( DIFFERENTIATE YOURSELF OR DIE)
Bill Gates anayefuata atatoka katika hicho unachofanya. Lakini sio tu kufanya kwa sababu kwa sababu unafanya bali kujitofautisha mwenyewe

Mark Zuckerberg anaweza kuwa mkulima. Lakini sio kwa tu kwa kulima kwa mazoea bali kwa kujitofautisha mwenyewe.

Larry Page na Sergie Brin wanaofuata sio kwamba watagundua Google search engine wanaweza kuwa wewe dereva. Kumbe jitofautishe mwenyewe ili uweze kufikia hatua hiyo kubwa.
RISE FROM ZERO TO ONE
RISE FROM VICTIM TO VICTOR
RISE FROM ZERO TO HERO

Anzia hapo ulipo.
Anza sasa.
Muda ni sasa
Badilika sasa.
Ishi sasa.
Fanya sasa.

Na GODIUS RWEYONGEZA
  Mwandishi
Coach
     0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X