Huwezi Kumkodisha Mtu Wa Kukupigia Push Up


Habari za leo rafiki yangu. Imani yangu kuwa umeamka vizuri asubuhi ya leo na unaenda kufanya makubwa.

Leo tuangalie jinsi ambavyo huwezi kumkodisha mtu kukupugia push up

Najua huwa unasoma vitabu na makala nyingi sana za kuelimisha na kukuhamamisha kila siku. Kama ulikuwa hujaanza kufanya hivyo anza leo.

Mambo yote ambayo unayasoma na kuhamasika hayatafanya kazi kama hutaanza kuyafanyia kazi.

Wanaokuelimisha hawawezi kuja kukufanyia kazi. Wewe ndiye unayepaswa kuchukua hatua na kusonga mbele.

Hakuna mtu ambaye unaweza kumkodisha akutengenezee _malengo._ Akutengenezee _master mind group_
Akuchagulie _mentors_
Akuchagulie _role models_
Akuandikie kitabu chako.
Wewe ndiye anayehusika na maisha yako hivyo chukua hatua muhinu sana.

Anza kutimiza wajibu wako, bila kutegemea kwamba kuna mtu wa kuna kukusaidia kupiga _push up_.

Wala hata sio serikali, wala sio walimu wako,
Sio rafiki zako. Hata sio wazazi.

Anza kupiga _push up_ zako. Namaanisha sasa hivi anza sasa.

Toka sasa hapo ulipo nenda hata ya ziada.
Toka sifuri uende moja
Toka chini upande juu
Toka chini upande hadi kileleni

Na
Rafiki yako
coach Godius Rweyongeza
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X