Ibua Kipaji Chako Sasa


watu wakisema hapana sio kwamba unakuwa umefika mwisho. Watu wakisema huwezi haimaanishi kabisa kwamba huwezi.

Ebu tujifunze kutoka kwa visa vya watu hawa wachache.

Soichiro Honda aliomba kazi kwenye kampuni ya TOYOTA lakini baada usaili hakupewa kazi.
Kukataliwa kwa Honda hakikuwa kikwazo bali chanzo cha kutoka sifuri kwenda moja. Alichokifanya Honda alianzisha kampuni ya kutengeneza baiskeli zenye injini ndogo Leo hii HONDA ni kampuni kubwa sana inayotengeneza magari na pikipiki.

Katika hali ya ubaguzi na kuteswa kwa watu weusi AFRIKA KUSINI ndipo alipoibuka Mandela na kuwa kiongozi mkubwa. Mandela anasema hivi “katika nchi yangu kwanza unakuwa mfungwa baadae unakuwa raisi”
Matatizo ya ubaguzi hayakuwa nafasi ya Mandela kusema siwezi kutoka sifuri kwenda moja.

Mambo  yaleyale yaliyotokea kwa mandela yanajitokeza kwa Nyerere. Katika shida ya ukoloni na kuteswa kwa watanzania kipaji chake cha uongozi kiliibuka.

Kumbe na wewe unaweza kuinua kipaji chako katika shida taabu kama hizo.

Kama hawa waliweza kuibuka baada ya kukataliwa na kuachwa basi na wewe unaweza.

Unachohitaji ni mtazamo chanya. Kuona chanya katika kila kitu ni muhimu.
Jifunze kutoka kwa watu hawa watu Wawili waliotumwa kwenda katika kisiwa kuangalia kama kampuni linaweza kutuma viatu kwenye kisiwa hicho.
Walipofika wakaona watu wanatembea peku.
Mtu wa kwanza akatuma ujumbe makao makuu ya kampuni kwamba waandae konteina tano za viatu,
 mtu wa pili akatuma ujumbe kwamba wasiandae hata kiatu kimoja maana watu wa eneo hilo hawana utaratibu wa kuvaa viatu.
Unaona hawa watu Wawili wana mtazamo tofauti. Mtzamo chanya na hasi.

Unahitaji kuwa na mtazamo chanya ili kuona uzuri katika ubaya. Kama ilivyokuwa kwa Honda, Nyerere na Mandela.
RISE NOW FROM ZERO TO ONE
RISE FROM VICTIM TO VICTOR
RISE FROM ZERO TO HERO
RISE FROM BOTTOM TO TOP

©songambele

Na
Coach Godius Rweyongeza
0755848391

godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X