Ruhusu kitu chochote kinachotokea kwako kitokee lakini pia ruhusu mambo yanayotokea kwa watu wengine yatokee.
Kama kuna kitu ambacho kinataka kutokea kwako usianze kukizuia ili kisitokee. Kama utapigana kwa nguvu yako kutaka kisitokee basi kitu hicho kitaendelea kitaendelea kuwepo.
Maana sheria ya asili ya uvutano ( _law of attraction_) inasema kwamba unavuta kwako Kile ambacho umewekeza nguvu sana).
Na kauli hiyo inaenda sambamba na kauli ya mwandishi maarufu Napolleon Hill anayesema Kile ambacho akili yako inaweza kubebelea na kuamini basi itakifikia
Hivyo kama wewe utaweka nguvu katika kukataza kitu kusitokee basi utapata hicho hicho ulichowekea nguvu. Kama ambavyo wahenga wetu walisema kwamba utavuna ulichopanda
Ruhusu na rafiki zako wapate wanachostahili kupata. Na wewe kubali kile ambacho ni cha kwako.
Na
Coach Godius Rweyongeza
0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com