Makosa Mawili (02) Ambayo Vijana Wanaoomba Kazi Wanafanya



Habari za siku ya leo rafiki na ndugu msomaji wa blogu yako ya songa mbele, Imani yangu kwamba leo ni siku bora na njema sana kwako. Unaenda kuweka juhudi na kuhakikisha kwamba umeweza kupiga hatua kubwa sana. Hakikisha kwamba unaweka juhudi na unafanya kazi zako kwa weredi wa hali ya juu sana ili uweze kufikia hatua kubwa sana.
Karibu tena katika Makala ya leo ambapo tunaaenda kujifunza makosa mawili ambayo watu wanaoomba kazi huwa wanayafanya kila siku. makosa haya yamewagharimu wanaoomba kazi wengi sana. Yanaweza pia  kukugharimu na wewe kama utaenda kuomba kazi bila kuhakikisha kwamba umeweza kuyafanyia kazi. Makosa haya  pia yanaweza pia kumgharimu rafiki yako ambaye anaenda kuomba kazi. Hivyo hakikisha kwamba utakapokuwa umejifunza makosa haya, basi unachukua hatua kutoyarudia makosa haya. Lakini kikubwa Zaidi ni kwamba unahakikisha kwamba unamshirikisha na mwenzako ili naye asije akafanya makosa haya. Siku zote unapojifunza kitu kipya hakikisha kwamba unawashirikisha watu wengine zaidi ya watatu ili nao wapate maarifa ambayo na wewe umeweza kupata. Isije ikawa kwamba wewe unapopiga hatua kuna watu ambao  ulipaswa kwenda nao ila kwa sababu tu hukuwapa maarifa ya kutosha basi wanakuwa chanzo cha kukkurudisha wewe nyuma. Hivyo baada ya hapa chukua link hii uwasirikishe watu watatu ili nao wajifunze  ulichojifunze.
1. KUTOMJUA MWAJIRI
Kosa kubwa ambalo watu hufanya wakati wa kuomba ni kutomfahamu vizuri yule ambaye wanaenda kumwomba kazi. Kwa kusoma linaweza kuonekana ni rahisi sana lakini kimantiki lina maana kubwa sana. Kama unaaenda kumwomba mtu kazi ambaye humjui bora usiende kabisa maana unapoteza muda wako.
Kumbe unahitaji kumjua yule ambaye unaenda kumwomba kazi. Anashughulika na nini? Kama ni kampuni inashughulika na nini? Ameanza kazi zake lini? Na taarifa nyingine za muhimu zinazomhusu yeye.
2. JUA AINA YA KAZI AMBAYO UNAEDA KUIOMBA.
Ni marufuku kufika kwa mtu amabye unaenda kukmwomba kazi na kumwambia kwamba mimi naweza kufanya kazi yoyote. Waajri hawatafuti watu ambao ni general bali wanatafuta watu ambao ni specific. Hivyo unapaswa kujua kwamba wewe ni msaada sehemu gani na unaweza kumsaidia nini yule ambaye unaenda kumwomba kazi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X