Mambo Saba Unayohitaji Kuyajua Ili Kuucheza Mchezo Wa Maisha Vizuri.


Habari za siku ya leo rafiki na ndugu msomaji wa blogu hii ya songa mbele. Imani yangu kwamba siku yako umeianza vyema sana na unaenda kufanya mambo makubwa sana ndani ys siku hii ya leo.
 Image result for football goal
Watu wengi sana wanachukulia maisha kama vita (mapambano), lakini sio kweli kwamba maisha ni mapambano.
Maisha ni mchezo ambao huwezi kuucheza kwa mafanikio bila kujua kanuni. Kama ilivyo kweli kwamba katika kila mchezo huwa kuna kanuni zake ndivyo ililvyo kweli kwamba katika mchezo wa maisha kuna kanuni mbali mbali. Endapo utazijua kanuni hizi basi utaweza kuucheza vizuri mchezo huu na kuushinda.
Siku zote mchezaji bora ni yule ambaye anazijua kanuni za mchezo husika na kuhakikisha kwamba amezifuata. Usipozifuata kanuni hizi za mchezo huu wa maisha jua kwamba lazima utakuja kuadhibiwa. Kama ilivyo kweli kwamba usipozifuata kanuni za mchezo wowote ule, uwe wa miguu, kikapu, tenisi, mpira wa wavu kutaja ila michache utaadhibiwa. Katika mpira wa miguu ukishika mpira katika eneo la hatari (ndani ya kumi nane) basi lazima utaadhibiwa tu.
Na yule ambaye umemchezea vibaya atapata penalti. Kama alliyepewa kucheza penalti hii ni mtaalamu basi jua kwamba atakufunga na hapo utakuwa unaelekea kupoteza mchezo.  Mchezo wa maisha nao uko kwa namna kama hiyo. Ukiufahamu jinsi ulivyo, basi utaweza kuucheza vizuri sana na kuweza kufikia hatua kubwa sana ya kimafanikio. Maisha ni mchezo, basi zifahamu kanuni zake nawe utafaidika sana.
1.   Hakuna kitu kikubwa sana kama kutoa kabla ya kupokea. Unapata kile ambacho unatoa. Ukitoa upendo utapokea upendo, ukichukia utachukiwa, ukipenda utapendwa., ukidanganya, utadanganywa pia.Nakubaliana na ZIG ZIGLER aliyewahi kusema kwamba “naweza kupata chochote kile ninachohitaji maishani kama nitawasaidia watu kupata kile ambacho wanakihitaji”.

Kumbe hapa ni muhimu kujua kwamba maisha sio tu kwamba yanakuhusu wewe bali maisha ni pamoja na wale ambao wamekuzunguka.

Unawasaidiaje watu waliokuzunguka kupata wanachotaka? Kwenye kitabu hiki cha MAISHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUEBE nimeelza kwa kina vitu unavyoweza kufanya, vikaongeza thamani kwenye maisha ya watu wengine na kuwafanya kuwa bora zaidi.

Pata nakala yako sasa kwa kuwasiliana nami kwa 0684408755 kupata nakala yako.
Nakala ngumu ni 25,000/-
Nakala laini ni 10,000/-
Na nakala ya sauti ni 10,000/-

Wewe unalipia ipi?

Tumia lipa namba ya Voda ambayo ni 5564517 jina ni GODIUS RWEYONGEZA

2.     Kile ambacho unaujaza ubongo wako muda sio mrefu kitajionesha kwa nje.  HaPo ndipo NAPOLLEON HILL anakwambia kwamba “kile ambacho akili yako inaweza kushikilia na kukiamini, basi inaaweza kuifikia” kama itashikilia uovu basi jua kwamba utakuwa mwovu. Kama itashikilia wema basi jua kwamba utakuwa mwema.
Ili kuucheza vizuri mchezo huu wa maisha lazima uwe tayari kuwekeza vitu vizuri vinavyohusu utajiri, afya na upendo katika ubongo wako. Maana siku zote unavuna kile ambacho umepanda. Ukipanda wema utavuna wema. Ukiua kwa upanga utauawa kwa upanga.
3.     Ili  kuweza kuutengeneza kile ambacho unaujaza ubongo wako ni muhimu sana kufahamu kwamba ubongo wako umegawanyika katika sehemu tatu. SUB CONSIOUS, CONSIOUS na SUPER CONSIOUS. SUBCONSIOUS haina kitu chochote kile ila huwa inajaribu kuonesha kwa nje kile ambacho huwa unaujaza. Kama utaijaza sehemu hii ya ubongo  na mambo mazuri utaishia kupata mazuri tu. Na kama utaijaza na mambo mabaya, basi itakupeleka  na itajitahidi kuhakikisha kwamba inauona ubaya. CONSIOUS ndiyo hushughulika na mawazo yote mema kwa mabaya.
Hapo ndipo nakubaliana na maneno ya JAMES ALLEN aliyesema kwamba “leo upo hapo ambapo mawazo yako yamekuleta, kesho utakuwa pale ambapo mawazo yako yatakupeleka”. Ni muhimu pia kufahamu kwamba ni sehemu hii ya ubongo ambayo huwa inaijaza subconscious chochote kile kupitia mawazo yako na fikra zako. SUPER CONSIOUS ni sehemu ya ubongo wa kimungu na unashughulika na mambo ya kiroho. Huku ndiko kuna kitu kile ambacho unaweza kukifanya ambacho mtu mwingine hawezi kufanya. Usipoitumia sehemu hii vizuri, basi utaishi maisha bila kufanya kile  ulipaswa kufanya. Naam, utafanya kile ambacho hutaki na hufurahii.
4.     Maneno yako ambayo unayaongea yanaweza kukuinua au yanaweza kukuangusha.
Maneno yanaweza kukujenga au kukubomoa. Hakikisha kwamba unapangilia maneno yako ambayo unayaongea. Kama unaona hakuna ulazima wa kuongea ni bora ukakaa kimya, kuliko kuongea na kuharibu heshima na hali au mazingira ya eneo husika. Unapaswa kuwa na kauli za kishindi wala sio kauli za kushindwa. “mshindi siku zote anasema kwamba ni jambo gumu lakini linawezekana. Mshinde anasema kwamba linawezekana lakini ni jambo gumu” alisema PADRE DAKTARI FAUSTINE KAMUGISHA katika kitabu chake cha Maji yakimwagika yanazoleka.
5.     Siku zote kila kitu kipo cha kutosha, unaweza kupata kile ambacho akili yako itajitahidi kuona. Kama akili yako itajitahidi kuuona ubaya basi kweli ubaya utajitokeza kwa nje. kama akili yako itajitahidi kuuona wema basi wema utaonekana. Kama akili yako itauona utajiri basi utajiri utajionesha kwa nje. na kama akili yako itauona umaskini basi utajionesha kwa nje. ama kweli maisha ni mchezo.
6.     Kama utatamani kitu bila kuogopa. Unaweza kukipata  kile kitu. Watu wengi wamejazwa na uoga wa kila aina. Uoga wa kuongea, uoga wa kufanya n.k, ebu achana na uoga na anza kuwa wewe. Anza kuishi kwa namna ambayo wewe unataka na anza kufanya kile ambacho unaona kwamba unapaswa kuwa umefanya. Uoga sio kitu kingine tofauti na ile hali ambayo wewe huwa unaitengeneza katika akili yako. kama hali ya  kuogopa utaipa nafasi kubwa sana katika maisha yako, basi jua kwamba unajididimiza. Usikubali hata siku moja ukatawaliwa na hali hii ya uoga. Maisha ni mchezo na wewe ndiwe mchezaji hakikisha kwamba unaucheza vizuri sana.
7.     Unaweza kuuondoa uoga katika maisha kwa kuwa na imani. “Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana” (Waebrania 11:1) kuwa na imani juu ya kile ambacho unafanya. Kuwa na imani na wale ambao unafanya nao kazi, kuwa na imani kwamba utapata kile ambacho unafanya tena utakipata kwa ubora wa hali ya juu sana. maisha ni mchezo. Ucheze vizuri sana mchezo huu ili uweze kushinda.
8.     Hakikisha kwamba unaondoa hasi zote katika ubongo wako.  Iwe umeziweka kwa kujua au kwa kutokujua. Iambie akili yako kwamba sasa naziondoa na kuzichoma katika shimo la takataka hasi zote ambazo zinautawala ubongo wangu!  Sasa nakaribisha rekodi za uchanya. Rekodi za ushindi, wema, utajiri, afya njema,busara na uzuri. Maisha ni mchezo. Ucheze salama ili uweze kufanikiwa.
Ni muhimu sana kufahamu kwamba mchezo huu wa maisha ushaanza tangu siku ulipozaliwa.  Kama bado unasubiri refa wa kuja kukupulizia kipenga ili ukaucheze mchezo huu jua kwamba unajichelewesha wewe mwenyewe. Kile ambacho unakifanya siku hii ya leo ni sehemu ya mchezo huu mzuri wa maisha. Maisha ni mchezo hakikisha kwamba unaucheza kwa ustadi wa hali ya juu sana. mwisho wa siku mshindi sio yule mtu ambaye yupo tu na ametulia. Bali ni yule ambaye anapigana kuhakikisha kwamba anafika kule ambapo anataka kufika. Maisha ni mchezo. Ucheze kwa ustadi.

Nakushukuru sana kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X