NIMEZALIWA MSHINDI; AMUA➡AMINI➡PATA


“napoamua kwamba nitafanya kitu fulani, inatosha, maana uamuzi huwa unafanya Mara moja tu’ alisema Tonny Robbins mwandishi na mjasiliamali wa kimarekani.

Kwa kitu chochote Kile unachotaka uamuzi huwa unafanyika Mara moja.

Ndio maana ukienda dukani kununua kitu hurudii rudii kitu kilekile Mara kwa Mara.

Bali ukisema niletee nguo fulani basi unakuwa umemaliza.

Au ukifanya muamara wa MPESA, huwa haurudii mara kwa Mara kutoa pesa ili ifike kwa wakala. Ukitoa umetoa basi, hakuna cha ziada.

Kumbe hata wewe kama una tabia fulani unataka kuacha ukisema naacha inatosha.

Kama kuna tabia unataka kuwa nazo ukisema kuanzia leo nitaishi maisha hata, basi inatosha.

Ukisema sivuti tena sigara, au madawa ya kulevya hakuna tena haja kuanza kujifikiria Mara mbili Tatu kama umeacha kweli au la

Kinachofuata baada ya kuamua ni kuamini kwamba Kile kitu tayari unacho mkononi mwako.
Anza kujiona tayari unamiliki Kile kitu.

Kwa namna moja au nyingine ukianza kujiona kama hufai kuwa na Kile kitu, kweli utakuwa hufai.
Kama utajiona Kile kitu sio cha viwango vyako, kweli sio cha viwango vyako.

Imani ni msingi mkubwa sana katika kupata Kile unachotaka.

Nilipoingia kwenye mistari ya biblia nikakuta haya juu ya imani.

Marko  11:24 kwa hiyo nawaambieni, mnaposali na kuomba kitu, aminini kwamba mmekipokea nanyi mtapewa

Matayo 21:22 mkiwa na imani chochote mtakachoomba mtapata

Amua amini pata.

Kumbe baada ya hapo kinachofuata ni kupata.
Sasa nitapataje?
Usianze kujiuliza swali hili maana litaanza kukuletea hofu na kujikuta unachoamini hakiwi.
Bali fanyia kazi vitu ambavyo vinakuja kwako kupitia Kile ambacho akili yako!!

Linaweza kuwa ni wazo juu ya kitu fulani badala ya kuanza kulihoji mara kwa mara. Anza kulifanyia kazi.

Na
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X