NIMEZALIWA MSHINDI; Hii Ndiyo Sehemu Bora Unapopaswa Kuwa


Kuna MTU mmoja aliwahi kusema kwamba “kama wewe kwenye chumba chako ndio MTU pekee ambaye ana busara sana basi jua kwamba unapaswa kutoka kwenye chumba hicho na kutafuta chumba kingine, maana haupo kwenye eneo sahihi”.

Kumbe kama wewe ndiwe MTU ambaye anategemewa sana kwenye eneo ulilopo na unaonekana kama MTU mwenye busara sana kuliko watu wengine kwenye eneo hilo jua kwamba haupo eneo sahihi hata kidogo.

Eneo zuri ambalo unapaswa kuwa ni lile ambalo utakuwa umezungukwa na watu makini sana zaidi yako. Watu ambao wana uelewa mkubwa sana zaidi yako na watu ambao wanafikiri vizuri na kwa namna ya tofauti zaidi yako.  Kama unataka kuwa MTU wa kufanya kwa namna ya tofauti. Jizungushe na watu wenye uelewa zaidi Yako. Donald Trump aliwahi kuandika kwamba rafiki zangu ni wale ambao wana uelewa mkubwa zaidi yangu na hao ndio watu ambao ninafanaya nao kazi.
Ushauri huu ni wa kweli na una maana kubwa sana kwa ulimwengu wa sasa hivi.

Hatua ya kuchukua sasa. 
Hakikisha kwamba unatafuta na kukaa sehemu ambapo kuna watu wenye uelewa, ujuzi, na ufahamu mkubwa zaidi Yako. Usikubali kukaa na watu walewale wanofanya vitu kwa namna ya kawaida na kulalamika mara zote. Kama watu wa namna hii huwapati, basi fanya vitabu kuwa rafiki wa kweli.
Mimi nataka kukaa na watu makini wewe Je?
Tukutane kileleni


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X