Kadri siku zinavyozidi kusonga mbele vitu navyo vinazidi kushuka na pengine vingine vinazeeka. Vipo vingine vinavyotoweka kabisa katika ulimwengu huu na kutoonekana. Mfano kuna wanayama ambao wanaitwa dinosaurs wanyama hawa wametoweka kabisa kwenye uso wa dunia na hawaonekani kabisa. Leo imebaki kuwa historia kwamba walikuwepo basi hauna mingine cha ziada. Labda tu pengine kuonekana kwenye movie na maigizo mbali mbali.
Lakini pia kuna mimea ambayo nayo imetoweka kabisa kwenye USO wa dunia na kubaki kuwa historia. Kuna aina nyingi sana za mimea ambazo zimetoweka.
Jua nalo lipo kwenye kuungua kila siku, kitu ambacho kinalifanya jua nalo kuzidi kufifia kadri ya umri. Kama ambavyo mtu mmoja aliwahi kusema “nyota zitatoweka na jua nalo hufifia kadri siku zinavyosogea” lakini kuna mtu mmoja ambaye hata iweje hawezi kufifia wala kutoweka wala kupotea kabisa kwenye uso huu wa dunia.
Mtu huyo ni WEWE. Wewe ni kiumbe ambacho kina nguvu na uwezo wa kukua na kuhakikisha kwamba hakitoweki kwenye uso wa dunia hii.
Wewe una uwezo wa kukua na kuhakikisha kwamba hautoweki kwenye uso wa dunia hii kama utaweka juhudi na nguvu kubwa sana katika kuhakikisha unafanya yafuatayo.
1. Haushindwi na kukatishwa tamaa na vikwazo vidogo ambavyo unakutana navyo kila siku kwenye maisha yako. Kupambana ni wajibu wako. Lakini pia kuhakikisha kwamba unashinda ni wajibu wako. Weka sana juhudi katika kuhakikisha kwamba unaweza kushinda katika mambo madogo ambayo unafanya kila siku. Hata kama vikwazo ni vikubwa, jua kwamba ushindi ni wajibu wako. Wewe umezaliwa mshindi. Wewe ndiwe mtu ambaye unapaswa kuhakikisha kwamba unashinda na unaenda hatua ya ziada katika kila kitu unachofanya.
Pangilia ratiba Yako vizuri sana siku hii ya leo ili baada ya hapa uende kushinda katika Kile ambacho utafanya siku hii ya leo.
2. Unaanza kufanya kitu ambacho kitazidi kuwepo miaka kadha wa kadha baada ya wewe kuanzisha kitu hicho. Fanya kitu ambacho kitakuwa msaada mkubwa sana kwako na kwa watu wengine ambao wanakuja mbele yako. Kuna watu ambao walianzisha vitu miaka mingi sana ila mpaka sasa hivi vitu hivyo vipo, naam kumbe nao bado wanaishi kwenye ulimwengu huu.
3. Unaandika Kitabu.
Moja kati ya vitu ambavyo unaweza kufanya na visitoweke hapa duniani ni kuandika Kitabu. Kitabu kinaweza kudumu kwa miaka mingi sana. Kuna vitabu ambavyo watu waliviandika kabla ya kristo mpaka sasa bado vipo na vina msaada sana. Vitabu vya watu hao vinawafanya watu hao waishi kwenye ulimwengu huu.
4. Utapanda mti.
Miti inaweza kupandwa na kuendelea kuwepo kwa miaka mingi sana zaidi ya 100. Watu watakuwa wanakumbuka kwamba miti hii ulipanda wewe hapo. Na isitoshe unapopanda miti bado unakuwa umetunza mazingira.