NIMEZALIWA MSHINDI: IJUE KANUNI YA PASI NA HAKIKISHA UNAITUMIA


Habari za siku hii ya leo rafiki yangu na ndugu msomaji wa makala za songa mbele blog. Leo ni siku njema sana kwetu na tunaenda kuweka juhudi kubwa sana kuhakikisha kwamba tunaweza kufikia mafanikio makubwa sana.
Kumbuka kwamba leo ni siku ya tofauti na siku nyingine ambazo umewahi kukutana nazo maishani mwako. Weka juhudi kubwa sana leo kufanya kilichobora kwa ajili ya maendeleo yako binafsi.

Ndani ya siku hii ya leo napenda ujifunze kanuni ambavyo inatumiwa na pasi na vyombo vingine vya moto. Bila shaka umekuwa ukitunia Paso ya umemem kila siku lakini hujawahi kugundua hili.

Unapowasha pasi ya umeme inatumia umeme mwingi kuwaka na kupata joto kuliko inavyotumia umeme baada ya kupata joto.
Au kwa lugha nyingine ni kwamba ndani ya muda mwingine wa kupiga pasi baada ya kupata joto pasi hutumia umeme kidogo kuliko nguvu ya umeme iliyotunika kuiwasha.

Usishangae huu ndio ukweli.
Lakini kanuni hii haishii tu kwenye Pasi. Bali hata kwenye vyombo vingine vya usafiri. Mfano mafuta yanayotumika kuliwasha na kuliondoa gari ni mengi sana kiasi kwamba yanazidi Yale ambayo yanalifanga liendelee na safari.

Sasa hii maana yake nini?

Ndio najua utakuwa umejiuliza hilo swali. Hii ina umuhimu mkubwa sana kwenye maisha yetu.

Shughuli yoyote ile utakayoianza lazima itachujua muda kabla ya kujengeka na kuwepo. Hivyo kama kuna kazi ambayo unaianza, usichoke kuweka nguvu yako huko. Jitahidi upige kazi kwa bidii huku ukiipa muda maana ni kanuni ya maisha kwamba itafikia wakati itakua na kuanza kuhitaji nguvu kidogo.

Tukutane kileleni.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X