Wahenga walisema kwamba meneno huumba. Hii ni kauli muhimu sana ambayo unahitaji kuifahamu na kuitumia kwenye maisha yako kwa ajili ya kupata kilichobora.
Kila kauli unayoitoa huwa inaleta madhara yake, kwako.
Ukisema kwamba kwa hakika hili siliwezi, basi umemaliza. huliwezi kweli!
Ukisema mimi ni mjinga, ni kweli wewe utakuwa mjinga.
Kumbe kama maneno yanaumba basi tuzitafute kauli nzuri ambazo tutajisemea sisi wenyewe kila wakati. Kauli nzuri, kauli za kukujenga.
Kwa mfano binafsi nafahamu kwamba
Utajiri wote umeumbwa kwa ajili yangu
Vitu vizuri vimeumbwa kwa ajili yangu
Mimi ni mshindi
Mimi nastahili kupata kilichobora
Mimi ni mtu anayeng’aa katika kila sekta.
Ebu na wewe niwekee kauli zako hapa nizione๐๐ฟ๐๐ฟ๐๐ฟ๐๐ฟ
Na
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391