NIMEZALIWA MSHINDI; Mambo Manne (04) Yatakayokufanya Ung’ae


Kama Unataka kuwa millionea lazima ufanye ambavyo mamilionea wanafanya. Kama unataka kuwa mwanamziki lazima ufanye kama ambavyo wanamziki wanafanya.

Watafute watu ambao unaona kwamba wao wamefanikiwa katika sekta ambayo na wewe unataka kung’aa ili na upate sehemu nzuri ya kuanzia. Angalia wanafanya nini ila hakikisha kwamba unajitofautisha wewe mwenyewe na kufanya kwa namna ya tofauti. Jitofautishe kwa kufanya kazi za tofauti, maana wewe ni wa tofauti sana.

Hakikisha kwamba wewe unajitofautisha sana maana kama utafanya kama ambavyo kila mmoja aliyekuzunguka anafanya basi na wewe hautakuwa na tofauti na hao wengine.

Haya hapa ni mambo matano ambayo yatakufanya ung’ae haraka sana kwenye sekta yako.

1. Umakini wako wa kufanya kazi.
Kama unafanya kazi yako kama ambavyo kila mtu anafanya basi jua kwamba upo njiani kupotea.

Hakikisha kwamba unapoanza kufanya kazi yako unashughulika kwa kiwango cha juu sana ili uweze kuifanikisha kazi yako. Ifanye kazi yako kwa akili yako yote. Kwa kipindi ambacho utakuwa unafanya kazi hiyo, hakikisha kwamba akili yako ipo hapo na haiami kabisa. Siri kubwa sana ya mafanikio ipo katika kufanya kazi kwa umakini

2. Maliza.
Usianze kufanya kazi na kuishia tu njiani. Hakikisha kwamba unaenda hatua ya ziada kwenye utendaji wako na kuhakikisha kwamba unaweza kufikia mwisho wa ile kazi yako. Kuna raha kubwa sana katika kumaliza. Usifanye vitu nusu, nusu. Fanya kwa kumaliza.

3. Jifunze kutokana na makosa.
Kila siku kwenye kazi yako kuna mambo mapya ya kujifunza. hakikisha kwamba umejifunza mambo mapya kila siku. Yafanyie kazi Yale yote ambayo unajifunza kila siku.
Kila changamoto kwako iwe ni somo zuri la kukupeleka kwenye mafanikio.
Jifunze, jifunze jifunze.

4. Watafute watu sahihi.
Kama ambavyo nimetangulia kuandika mwanzoni mwa makala haya. Kama unataka kuwa  milionea lazima uwatafute mamilionea wengine wakupe mbinu za kimilionea. Ukikaa na watu wa kawaida, watakuangusha na kukurudisha chini.

Swali la hapa ni Je, nitawapata wapi mamilionea?
“ndege wa rangi moja huruka pamoja” ni methali ya wahenga.

Ili uweze kuwapata hawa mamilionea unahitaji kufanya mambo yafuatayo.

Moja unahitaji kuwa na nia ya dhati ya kuhakikisha kwamba unafanikiwa  na kuwa milionea

Pili unapaswa kuwa na mpango madhubuti ambao unaufuata kila siku.

Tatu, unahitaji kusoma na kujifunza kila siku kutoka kwa hao mamilionea.

Soma vitabu vyao, sikiliza audio book za maana kutoka kwao.
Kusoma vitabu kutakufanya uongee na watu hao.

Kumbuka kwamba “ukifikiria mazuri, mazuri yatakufuata na ukifikria mabaya jua kwamba mabaya yatakufuata” ni maneno ya Joseph Murphy

5. Ugumu wa wewe kusimamishwa au kuondolewa kwenye kiti chako
Kama unafanya kazi kwa bidii na na kutoa thamani ambayo hatoi mtu mwingine basi wewe upo vizuri. Ila kama kile unachofanya tunaweza kukipata sehemu nyingine basi jua kwamba unapoteza.
Watu wanaong’aa katika sekta zao sio watu rahisi sana kuwa replaced. Hivyo watu hao wamehakikisha kwamba wanafanya yafuatayo.

Moja wanatoa thamani kubwa sana kwenye kazi yao.

Pili wanaifanya kazi yao bila ya kuweka vikwazo

Tatu hawawabebeshi majukumu  watu wengine kama wanajua kwamba wao ndio wahusika wakuu

Nne, Kile kinachitoka mkononi mwao wanakuwa wamejiridhisha kwamba wamekifanya kwa nguvu na akili yako kwa kiwango cha juu sana.

Fanyia hayo kazi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X