NIMEZALIWA MSHINDI; MAWAZO—–>HISIA—>MTENDO—–>MATOKEO


Habari za leo Rafiki yangu. Imani yangu umeianza wiki hii vyema ukiwa unaenda kufanya makubwa sana wiki hii.
karibu sana

Leo hii tutafakari hiki kitu

Thoughts ➡feelings ➡actions➡results

Kila kitu ambacho unacho katika maisha yako umekivuta kwako kwa mawazo yako ambayo unafikiria. Kiwe Kizuri au kibaya. Mawazo ndiyo hupelekea hisia zako unazopata. Kumbe hisia zozote utakazopata leo ni kwa sababu umezipata kutoka kwenye mawazo yako. Hivi sasa hivi una hisia gani? Unaweza kutulia kidogo kujiuliza swali hili.

 Hisia hutupelekea kufanya vitu(actions) mbali mbali. Kwa hiyo kama hisia zako ni chanya zitakupelekea kufanya vitu chanya. Kama ni hasi utafanya mambo hasi.

Lakini pia kufanya ndio hutuleta kwenye matokeo. Hisia chanya huleta matokeo chanya na kinyume chake ni sahihi. Lakini yote chanzo chake ni mawazo yako.

Kumbe kama huoni matokeo mazuri jua kwamba huna mawazo mazuri. Kama unaona matokeo mazuri jua kwamba umeyavutia kwako kwa mawazo mazuri

Kanuni hii inafanya kazi uwe Tanzania, Ulaya, amerika, urusi au China.

Inafanya kazi uwe hata kama umelala, upo macho, upo safarini au umetulia, kaskazini au magharibi.

Inafanya kazi na siku zote huwa haijichanganyi. Ni kama sheria ya uvutano(gravity)

Ukidondoka gravity haijui wewe ni mtu mwema au mbaya.
Wala haijawahi kutokea hata siku moja kwamba gravity imesahahu kufanya kazi. Yaan siku hiyo nguruwe wakaruka angani na kutua chini.
Gravity inafanya kazi muda wote kwa watu wote vivyo hivyo kanuni hii ambayo huwa napenda kuiita kanuni ya UTAVUNA ULICHOPANDA.

Mambo muhimu ya kufahamu.
1. Mawazo yako huwa vitu.
2.,mawazo yako ya sasa yanatengeneza maisha ya baadae.
3. Vitu vinavyofanana siku zote huja pamoja.
4. Wewe ni mnara mkubwa sana ambao haujawahi kutengenezwa hapa duniani. Hivyo safirisha mawimbi sahihi.
5. Wewe ni sumaku kubwa sana na hakuna sumaku ambayo imetengenezwa yenye uwezo wa kuvuta kama wewe. Anza kuvuta vitu vizuri kwako.

www.songambeleblog.blogspot.com

Ni Mimi
Coach Godius Rweyongeza
O755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X