NIMEZALIWA MSHINDI; NI BORA KUOMBA SAMAHANI KULIKO KUOMBA RUHUSA..


Moja kati ya vitu ambavyo unavihitaji katika dunia hii ni ubunifu. Nimegundua kitu ambacho kinawatofautisha waliofanikiwa na wale ambao  bado wako chini ni ubunifu.

Mara nyingi ubunifu huwa unatokana na mambo mawili

Moja, kile ambacho wewe unaona kwamba ni shida kwako ila ukikitatua unaona ni msaada kwako na kwa watu wengine.

Pili, shida ambazo zinawakuta watu wengine. Hivyo unaweza kutatua matatizo ya watu wengine kwa kuwa mbunifu.

Makala ya leo inatuambia kwamba ni bora kuwa NI BORA KUOMBA SAMAHANI KULIKO KUOMBA RUHUSA.

Kama kuna kitu kipya ambacho unahitaji kufanya, usianze kuzunguka na kuomba ruhusa kwa watu badala yake nenda kafanye Kile kitu kwa ubunifu. Tena kifanye kwa ubora. Kama itatokea kwamba unachotaka kufanya hakijafanikiwa unaweza kuomba samahani kwa wale ambao hawakupenda Kile kitu ambacho ulifanya. Ila kama mambo yataenda vizuri, basi hapo hakuna haja ya wewe kuanza kuomba samahani. Maana kila mtu atakiona kwamba ulichofanya ni chema sana.

Hivyo basi unapotoka hapa katumie hazina ya ubunifu ambayo imo ndani yako, kujaribu kufanya vitu vipya. Hakuna kitu kinaumiza kama kuwa na akiba ipo na hauitumii hata kidogo.

Kama kuna hatua Mpya ya kuchukua kifanye sasa. Ni bora kuomba samahani kuliko kuomba ruhusa.

Fanya maamuzi ya kiuwekezaji kama hayataenda vizuri basi baadae unaweza kubadilisha na na kufanya uwekezaji mwingine.  Na hapo utakuwa umejifunza mengi sana


One response to “NIMEZALIWA MSHINDI; NI BORA KUOMBA SAMAHANI KULIKO KUOMBA RUHUSA..”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X