NIMEZALIWA MSHINDI; Nje Au Ndani? Wapi Panafaa Zaidi?


Tunaishi katika dunia ambapo kila kitu kinapatikana kwa uwili. Yaani vitu vitu vingi vinaenda vikiwa na pande mbili mbili.

Mfano huwezi kuzungumzia mbele bila kuzungumzia nyuma,
Huwezi kuzungumzia juu bila kuzungumzia chini
Huwezi kuzungumzia kulia ukasahu kwamba kuna kushoto
Huwezi kuzungumzia urefu ukasahau ufupi.
Ukizungumzia juu ya suala la kukumbuka huwezi kusahau kwamba kuna kusahau,
Ukizungumzia unene basi jua kwamba hujaliacha mbali sana suala la wembamba.
Lakini pia ukizungumzia uzuri basi jua kwamba unakaribia kuuzungumiza ubaya

Yaani mlolongo wa aina hiyo upo mkubwa sana katika kila sekta na katika ila eneo. Vitu vingi vinaenda kwa uwili. Wengine wanapenda kuviita vinyume au opposites.

Suala hilo hajijaachwa nyuma haswa tunapozungumzia mafanikio na pesa kwa ujumla.

Kama ambavyo zipo sheria au kanuni za nje za kufanikiwa kama vile kuchapa kazi, kuwekeza, kutumia muda kuangalia uwekezaji wako na kuuza( MAUZO). Vivyo hivyo kuna sheria za ndani zinazohusu mafanikio, ambazo unahitaji uzibadili ili kuweza mafanikio ya nje.

Mara nyingi sana mafanikio ya nje yanachangiwa sana na kile ambacho MTU unakuwa nacho kwa ndani.

Kama ndani mtu una mtazamo wa kimasikini basi nje tunategemea kupata tabia za kimasikini. Kama ndani una mtazamo wa kitajiri basi nje utaonekana utajiri. Ni kwa mantiki hiyo usemi wa kiingereza wasema  Like produces lime. Usemj huu una maana kubwa sana.

Tunaishi katika dunia ya sababu na matokeo ambapo kila kitu kinachotokea kinakuwa kimesababishwa. Hakuna kitu kinachotokea kwa bahati mbaya hata siku moja.

Ukipanda mti, baadae ukaja kugundua kwamba matunda yake sio matamu na sio makubwa. Huwezi kukaa na kulalamika kwamba huu mti siupendi. Kwanza hautoi matunda mazuri na pili matunda yake sio matamu. Huwezi kufanya hivyo. Lakini unaweza kuubadili kwa kuhakikisha kwamba unapanda mti mwingine mzuri na wenye matunda bora na safi.

Unaweza pia kuamua kuurutubisha ili uweze kutoa matunda mazuri. Ndivyo ilivyo pia kwenye ulimwengu wa mafanikio na utajiri kiujumla.

Hivyo hapa mambo matatu ambayo unahitaji kuyabadili kwa ndani ili yakupe matokeo bora kwa nje.

1. Badili mtazamo wako juu ya pesa. Je, kwako pesa ina maana gani?

2. Badili msukumo wako juu ya pesa. Je, ni kitu gani kinakusukuma ili utafute pesa? Je, ni kwa sababu umezaliwa masikini na unauchukia umasikini? Au kwa sababu umekua unawaomba watu pesa wanakataa kukupa hiyo pesa sasa umeamua kutafuta pesa ili uwakomeshe?  Kitu Kizuri ambacho kinapaswa kukusukuma kutafuta pesa ni kusudi lako la maisha, huduma na upendo.

3. Unahitaji pia kubadilisha kauli hizo ambazo ulizisikia kipindi uko Mdogo sana. Kipindi Kile ambapo hata kama baba Yako angekukosea basi ulikuwa unakimbia chumbani kujifiicha maana hauwezi kumkalisha baba Yako chini na kuwambia shika adabu yako.

Fanyia kazi hayo ambayo umepata kujifunza hapa safuni kwa siku hii ya leo.
Usikose kuwashirikisha wenzako ili nao wapate Maarifa bora kama haya.

Hakikisha pia unajiunga na mfumo wetu maalumu wa kupokea MAKALA MAALUMU KWA WATU MAALUMU ambazo hutumwa  kila wiki.

BONYEZA HAPA KUJIUNGA.

Nakushukuru sana kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X