NIMEZALIWA MSHINDI: zaeni mkaongezeke
Mungu alipomuumba mwanadamau kuna baadhi ya vitu ambavyo alimkabidhi mwanadamu ili avitumie. Mungu alimpa manadamu uwezo wa  kuzalisha zaidi na kuviongeza zaidi vile ambavyo aliumba hapo mwanzoni. Kumbe wewe haujazaliwa kubweteka na kukaa tu huku ukiwa unataka kuishi maisha mazuri. Ebu mtazame MUNGU baada ya kumuumba Adamu. Alimwambia kwamba zaeni mkaongezeke. Tafsiri ya neno hili imechukuliwa vibaya na watu walio wengi na hivyo kujikuuta maana halisi ya kile ambacho kilikusudiwa mwanzoni kikipotezwa. Kumbuka kwamba MUNGU aliumba ardhi ila hakuumba chakula. Hivyo ni juu yako kuhakikisha kwamba unatumia juhudi zako ili kuweza kuzalisha chakula na kukiongeza. Unapolia njaa, ni kosa lako wala sio kosa la yule ambaye amkuumba wala mzazi wako. Ni muhimu pia kujua kwamba mzazi alipewa uwezo tu wa kukuleta duniani hakupewa mtoto. Ni kwa kutumia uwezo huo ameweza kukuleta hapa duniani. Kumbe kila mtu ana uwezo wa kuzalisha kitu chochote kile ambacho anataka katika maisha yake. Walio wengi wamejikita katika kuutumia uwezo wa kuongeza watotot tu na kusahau kwamba wanapaswa kuhakikisha kamba kuongeza vitu vingine. Mada kubwa sana inayoongelewa na watu haswa pale wanaposikia neno zani mkaongezeke basi ni kwamba ni kuongeza idadi ya watoto. Katika kila sekta bado kuna vitu vingi sana ambavyo vinapahitaji kuhakikisha kwamba vimeongezwa na kutengenezwa kwa namna yatofauti.
Kuna raslimali nyingi sana ambazo zimekuzunguka ambazo unapaswa kuhakikisha kwamba umeweza kuzitumia. Kama unalia maisha ni mabaya, huu ndio muda wako wa kujionea aibu. Wewe umeubwa kwa ajli ya kubadilishwa hasi kuwa chanya. Upo hapo ili uhakikishe kwamba unabadili ubaya kuwa uzuri na kuongeza uzuri zaidi. Upo hapo kuhakikisha kwamba unauoberesha uduni kuwa uimara. Mambo mazuri  yanapatikana kwa kufanya kazi na kutimiza amri ya MUNGU ya zaeni mkaongezeke. Yaani unapaswa kuwa mtu wa kuhakikisha kwamba unazalisha kitu kipya na kufanya vitu vya tofauti kila siku.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X