NMEZALIWA MSHINDI; Je, Wajua Kwamba Bahari Shwali Haitoi Wanamaji Stadi?


Siafu ni viumbe  wadogo sana, ambao huwa wanaonesha mfano mzuri sana katika ushirikiano na uchapaji kazi wake. Leo hii ningependa ujue kwamba kuna wakati siafu wanapokuwa wakisafiri, kuna baadhi ya siafu huwa wanalazimika kutengeneza nyumba kwa juu ili wenzao waweze kupita kwa chini.

 Sio kwamba wale wanaotengeneza hiyo nyumba kwa juu huwa wamekufa, hasha, bali ni kwamba huwa wanatengneza njia yao kuhakikisha kwamba wamejilinda. Lakini pia kujihakikishia kwamba adui wao hawawagusi na kuwaharibu.

siku zote nyakati ngumu huwa zina changamoto yake, lakini kila mtu huwa Anatafuta njia sahihi ya kuhakikisha kwamba ameweza kushinda na kwenda hatua ya ziada mbeleni. Ndio maana leo nikataka nikwambie kwamba BAHARI SHWALI HAITOI WANAMAJI STADI.

Sio huko tu ebu chukulia kwamba wewe leo hii ulikuwa unatembea shambani kwako. Mara ukafika sehemu na kuchomwa na miiba Mingi sana. Je, utafanyaje? Utaiacha ili siku nyingine ukija ikuchome au utaitoa?

Bila shaka utaiondoa kuhakikisha kwamba unaporudi kupita katika eneo hilo hauchomwi na miiba hiyo hiyo iliyokuumiza mwanzoni. Hivi ndivyo ambavyo maisha yanafundisha.
Maisha yanatengeneza mabaharia. Ila hayafundishi kwa kumkarisha MTU darasani na kuanza kumfundisha. Hapana, bali yanakupa vitu vya kufanya? Unapovifanya unakutana na changamoto. Ukiweza kuzitatua hizi changamoto basi wewe ndio mshindi na unakuwa Baharia aliyebobea. Bila changamoto hizi hakuna ukuaji, na bila ukuaji hakuna maendeleo. Ndio maana nikataka nikwambie kwambe kwamba, BAHARI SWALI SIKU ZOTE HAITOI WANAMAJI STADI.

Kama wewe unatafuta mteremko katika kufikia mafanikio, jua kwamba kuna kitu unakosea. Mafanikio hayatafutwi kwa kuchukua barabara rahisi ambayo haina makorongo, Bali mafanikio yanapatikana kwa kujifunza kupambana na vikwazo ambavyo vipo kwenye barabara hii ya mafanikio. Ukikutana na misumari kwenye barabara hii, ikusanye isije ikakuchoma tena.

Jifunze kuwa Baharia makini katika bahari ya mawimbi makali sana.

Ukitafuta  mteremko huwezi kutoka huko ukiwa Baharia au mwanamaji stadi.

 Nikutakie siku njema sana.

Kumbuka kwamba BAHARI SHWALI HAITOI WANAMAJI STADI!!!


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X