Ili kutoka sifuri kwenda moja mabadiliko ni kitu ambacho hakiepukiki.
Maana asili ya dunia ni kubadilika. Hakuna sehemu ambayo inabaki bila kubadilika au kuotesha kitu chochote.
Mfano mzuri ni ardhi. ukiilima ukaweka mazao yanaota na kutoa kile ulichopanda. Ukiiacha bila kuipanda basi jua kwamba bado kuna vitu ambavyo vitaota ambavyo ni magugu ingawa hukuvipanda.
Kumbe mabadiliko lazima yatokee iwe tumeyapanga au hatujayanga.
Akili yako ukiamua kuilisha kilichobora na kuifanya ifikrie kama ambavyo unataka wewe basi utakuwa umepanda kitu fulani lakini ukiiacha bila kuipa kazi lazima itajipa kazi kwa kukupa mawazo yoyote yale.
Lakini kwa wewe na Mimi lengo letu kubwa sana tuwe na mabadiliko chanya ambayo yatatufanya tutoke sifuri kwenda moja.
Basi ngoja tuzungumzie aina mbili za mabadiliko katika uzalishaji.
1. Mabadiliko ulalo
2. Mabadiliko wima
# mabadiliko mlalo
Mabadiliko ya aina hii hutokea pale kitu kitu kinapokuwa kimeshagunduliwa na wewe unakirudufu.
Mfano una kalamu moja na unazalisha kalamu mia moja.
Au
Una kikombe kimoja unazalisha vikombe vingine sabini.
Hayo ndiyo mabadiliko mlalo
# mabadiliko wima
Haya ni mabadiliko ambavyo hayatokei mara kwa mara ila ni mabadiliko yenye manufaa sana.
Mabadiliko haya yanaanzisha kitu kipya ambacho hakikuwahi kuwepo.
Yaani una kalamu unazalisha daftari.
Au
Una simu unazalisha laini.
Hayo ndiyo mabadiliko wima
Sasa unaenda kufanya mabadiliko gani?
Utasababisha mabadiliko gani leo?
Je unahitaji watu gani wa kufanya mabadiliko yako?
By
Coach Godius Rweyongeza
0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com