Fanya Haya Ili Uishi Milele.


Habari za leo rafiki yangu. Imani yangu siku yako umeianza kwa namna ya tofauti kabisa. Ikiwa ni siku njema sana kwako kwenda kufanya kitu ambacho ni bora sana kwenye maisha yako.

Leo hii tunaenda kuzungumzia kitu kingine ambacho watu huwa hawapendi kusikia kwenye masikio yao. Kitu ambacho watu wengi huwa kinawaumiza kichwa muda mwingi wakikifikiria. Kitu hiki kifo. Lakini sisi tunaenda kukizungumzia kwa namna ya tofauti sana. Wakati wengine wanogopa kufa, sisi tunajifunza kukimbutia kifo na kuishi milele. Kuna mtu mmoja aliwahi kusema kwamba wengi wetu watakufa lakini wachache sana ndio watakaoishi milele. Kumbe kama wengine wote watakufa basi Mimi na wewe tunapaswa kuishi milele. Amua leo kwamba unaenda kuishi milele kwa kufanya mambo haya hapa machache.

1. Anzisha kitu ambacho hutakimaliza wewe. Usiwe mchoyo. Fanya kitu ambacho wewe utafanya utawaachia watu wengine ili waweze kukiendeleza.

Kitu gani ambacho unaenda kufaya leo?. Alama gani ambayo unaenda kuweka siku ya leo?.  Je ni kitu gani cha kijamii ambacho unaenda kufanya leo.
Fanya kitu ambacho hutakimaliza leo.

2. Panda miti. Ukipanda miti leo, itachukua miaka kadhaa kuja kuuvuna, kizazi na kizazi kitafurahia miti yako ambayo unaipanda siku ya leo.

3. Andika kitabu. Kitabu ni raslimali ambavyo haizeeki. Ukikiandika leo, kitaishi miaka yote. Leo hii nasoma vitabu vya akina Socrates ingawa wameishi karne nyingi sana. Neweton mpaka leo hii anaishi kwa sababu ya vitabu alivyoandika bado anaishi. Njia nzuri ya kuongea na mtu ambaye ameishi miaka Mungu ya nyuma ni kuchukua kitabu chake na kukisoma. Na wewe amua kuishi milele.

Hayo ndiyo mambo matatu ambavyo unahitaji kuyafanya ili uweze kuishi milele.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X