Kuna watu ambao wanapenda sana kufanikiwa lakini hawachukui hatua, hata kidogo kuhakikisha kwamba wanatoka hapo walipo ili kwenda pale ambapoo wanatak kufika, kuna watu wana ndoto za kuanzisha biashara mpya lakini bado hawachukui hatua kila siku kuhakikish kwamba wanainuka. kuna watu ambao wao wanapenda kuwa viongozi wakubwa sana lakini hata hawachukui hatua za awali kkuhakikisha kwamba wanaweza kufika kule ambako wao wanataka kwenda na hatimaye kuweza kufikia mafanikio makubwa sana.
Acha kujihurumia! Chukua hatu mahususi kuhakikisha kwamba umeweza kufikia hatua kubwa sana. kama bado mpaka sasa unalala saa mbili na kuamka saa mbili nyingine huku ukijifariji kwamba lengo lako ni kuwa bilionea mkubwa sana duniani, naweza kukwambia kwamba hujachukkua hatua sahihi, za kukufikisha wewe kule ambapo unataka kufika. hatua sahihi ndizo unahitaji kuchukua. Moja ya hatua sahihi ambazo nakushauri uzichukue leo ni kwenda kusoma historia ya bilionea mmoja ili ujue kama na yeye huwa analala kama wewe. Chukua hatua sahihi leo ili uweze kufikia matokeo bora sana.
Kuna mtu mmoja ambaye alisema mimi nitakuja kuwa kiongozi mkubwa sana duniani. Rafiki yake alimuuliza ni hatua gani umechukua ili uweze kuwa kiongozi bora. Yule mtu alijibu mimi nipo tu nasubir siku yenyewe ikifika basi nitachaguliwa kuwa kiongozi na nitaanza kazi, nitalifanyia kazi hilo lengo langu.
rafiki yake alimwabia bado inaonekana hujajiandaa vyakutosha kuhakikisha kwamba unaweza kuwa kiongozi bora sana. Yule mtu hakuamini maana alitegemea kusifiwa kwa sababu kamba anataka kuwa kiongozi mkubwa. Lakini kutokana na ukweli kwamba rafiki yake alikuwa na uelewa mkubwa sana juu ya mambo ya uongozi ndipo alipomushauri mambo yafutato
1. soma sana watu wengine wanasemaje juu ya uongozi. jifunze kutoka kwa watu wengine ambao wamekuzunguka ili uweze kuinuka na kutoka hapo ulip na uweze kupiga hatua kubwa sana. (if you want to lead, read).
2. kuwa tayari kufanya kazi muda ule ambao wenzako wamepumuzika. kuwa tayari kufanya mambo ya tofauti wakati wengine wanaburudika.
kama una lengo la kujulikana kwa watu bilioni saba wa dunia hii, kuwa tayari kuchukua hatua leo ambayo itakufikisha kwenye mafanikio makubwa sana hapo mbeleni. anza hata kujenga utaratibu wa kuongeza mtu mmoja tu kila siku kwenye mzunguko wako wa watu wapya.
malengo yafanyiea kazi. achana na mambo ya kulala sana, achana na mambo ya kuhairisha kazi ambazo unatakiwa kuzifanya, achana na habari za kupoteza muda kufanya kazi ambazo hazikujengi kila siku. chukua hatu sasa kwa kufanya kitu cha tofauti.