HUU NI MUDA AMBAO UNAWEZA KUFANYA KILA KITU. Habari za siku ya leo rafiki yangu, imani yangu umeianza siku kwa namna ya tofauti na unaenda kufanya kitu cha tofauti. Leo hii ikiwa ni siku ya tarehe 17 June 2017. Tunaenda kujiufunza kitu kizuri sana. hakikisha kwamba unafanya kitu  na kukimaliza kile ambacho utakuwa umeanza kufanya siku ya leo hata kama ni kwa udogo. Hivyo utumie muda huu kuhakikisha kwamba umeweza kufanya mambo makubwa sana.
Katika siku za juma tunazo siku saba za wiki. Yaani tunayo jumatatu, jumanne jumatano, alhamisi,ijumaa, jumamosi, na jumapili. Hizi ni siku za juma ambazo dunia nzima zinafahamika. Hakuna sehemu ya nchi katika dunia hii ambayo ina siku zaidi ya hizo hapo. Wala hakuna sehemu ya dunia ambayo ina siku pungufu ya hizo hapo. Hakuna mtu ambaye mpaka sasa tunapoongea ameweza kugundua namna ambavyo tunaweza kuongeza hata siku, hali hii iko hivi  na itazidi kuwa hivi kwa muda mrefu sana. kumbe ni muhimu sana kwetu kuhakikisha kwamba tunaweza kuzitumia siku hizi saba za wiki.
Katika pitapita zangu na katika kuongea na watu mbali mbali nimegundua kwamba kuna siku ya juma ambayo watu wameiongeza. Sijui siku hii watu wameitoa wapi ndio maana mara nyingi sana huwa nakaa mdomo wazi nikisia watu wanaiongelea siku hii. Siku hii haipo kwenye hizo siku saba ambazo nimezitaja hapo juu. Siku watu wengi huwa wanapenda kuiishi. Hi siku hii hii ambayo inawafanya watu wengi sana wahairishe kazi kwa matumaini kwamba watakuja kuzifanya. Katika makala ya leo tunaenda kuiuzngumzia siku hii. Naamm siku hii inaitwa KESHO. Je,unaifahamu siku hii? Je,, umewahi kuiona siku hii? Je, umewahi kuiishi siku hii? Hii ndiyo siku yenye sifa ambazo nimeweza kzuitaja hapo juu.
Siku hii ndiyo inawafanya watu wengi sana kuhairisha kazi. ndio maana katika makala ya leo nikaipa kichwa cha HUU NI MUDA  AMBAO UNAWEZA KUFANYA KILA KITU. Ni kutokana na hali ya watu kuhairisha kazi na shughuli za muhimu kila siku na kuziweka kwenye siku ambayohaipo. Siku ambayo watu wengi sana wanaipenda kuiita kesho.
Muda mzuri wa wewe hapo kuhakikisha kwamba unafanya kazi ni sasa hivi. Usiaahirishe kazi zako leo na kusema kwamba nitazifanya kesho. Kesho haipo. Wala hakuna siku ya juma ambayo inaitwa kesho.
Kama kuna kazi au shughuli ambayo unahitaji kuifanya na mtu fulani,hakikisha kwamba mnaongea na mtu huyo husika na kupanga muda husika wa kufanya kitu hicho. Asikwambie tutufanya kesho. Ukiona mtu anakwambia kesho tutafanya kitu hiki. Ogopa sana. kataa. Ni bora sana mtu huyo akakwambia kwamba tutafanya jumatatu, au ijumaa kuliko kukwambia kesho.
Kuna msemo wa kisiswahili ambao unasema kwamba kesho huwa haiji. Tengeneza maisha bora muda huu ambao unasoma makala hii.
Naomba nikutakie muda mwema sana rafiki yangu. Maisha ni mzazuri sana hakikisha kwamba unayaishi. Maisha ni zawadi hakikisha kwamba unaitumi siku hii ya leo, maisha ni mziki hakikisha kwamba unaucheza mziki huu. Maisha ni chakula hakikisjhakwamba unakula chenye virutubisho. Utumie vizuri sana muda amabao unao siku hii ya leo ikiwa ni JUMAMOSI YA TAREHE 17 June 2017. Hakuna muda mwingine kama hu ambao utakuja kukutana no. amambo mazuri yanatengenezwa ndani ya siku hii nzuri sana.
Tukutane kileleni.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X