Maisha Unayaonaje -1


Hili ni swali la muhimu sana ambalo endapo utwauliza watu mbali mbali basi tegemea majibu tofauti tofauti kama ambavyo unakuwa umewauliza watu tofauti tofauti.

Yaani kila mtu ana mtazamo wake na ana jambo lake la kusema juu ya maisha.

Wapo wanaosema kwamba maisha ni majaribio, wengine wanasema maisha ni somo, wengine wanasema maisha ni mchezo lakini pia wengine wanasisitiza kwamba maisha ni zawadi.

Wale wanaosema kwamba maisha sherehe basi kwao kusherehekea kila siku ni kawaida!

Wale wanaosema kwamba  maisha ni mchezo kwao kushinda ndio jambo la msingi.

Wale wanaoona maisha kama mbio basi kwao harakani kitu cha lazima

Wale wanaoona maisha kama fiesta basi wao kuzunguka huku na kule ni sehemu ya ratiba yao ya kila siku.

Wewe maisha unayaonaje sasa?

Nitaomba uniwekee maoni yako hapa chini ili tuyajadili.

Ila maisha tunaweza kuyaona katika misingi mikuu mitatu.

1. Maisha kama majaribio
2. Maisha kama makabidhiano
3. Maisha kama  kazi ya muda ya kufanya ( temporary assignment)

maisha kama majaribio
Je, ni kweli maisha ni majaribio.
Ndio.
Katika kona ya biblia tunakutana na watu mbali mbali waliojaribiwa kwa nyakati tofauti tofauti!

Wapo walioshinda majaribio hayo na wapo waliofeli kabisa.

Abraham alijaribiwa alipoambiwa amtoe mwanae Isaak sadaka. Na alishinda jaribio hilo

Jacob alijaribiwa alipopaswa kufanya kazi miaka saba zaidi ili ampatae mke wake kipenzi Rachel. Na alishinda.

Katila Kurasa za biblia pia kuna watu wengine wengi waliojaribiwa na kushinda mfano wa hao watu ni Yosefu, Daniel, Ruth kutaja ila wachache.

Wapo pia walioshindwa majaribio hayo.

Adam na Eva walishindwa jaribio kutoka kwa Mungu wakiwa kwenye bustani ya Edeni.

Daudi alishindwa majaribio kutoka Kwa Mungu kwa nyakati tofauti tofauti.

Kumbe kama maisha ni majaribio basi tutegemee majaribio ya hapa na pale kila siku.

Ukweli ni kwamba hatujui jaribio gani Mimi na wewe tutapata, ila majaribio yapo.

Ila uhakika ni kwamba jaribio lolote halikuachi kama ulivyo,
Au litakuimarisha au kukudhoofisha.

Hatujui litakuja lini na katika jambo gani, ila matendo yetu kwa Yale mambo tunayoyafanya ndio yatayotupa majibu na kufanya matokeo kuwa hasi au chanya.

Kwa sasa naweka kalamu chini baadaee nitaeleza kwa undani maisha kama makabidhiano

Na

Coach Godius Rweyongeza
Mwandishi

Email_godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X