Maisha Unayaonaje? -2


Hodi hodi tena hapa safuni. Narudi tena uwanjani kujimwaga na kuendelea na mada yetu ambayo siku ya jana tumeigusa kidogo.

Jana tumezungumzia na kuangalia ni kwa jinsi gani tunapaswa kuayaangalia maisha kama majaribio. Kwa mifano niliyotoa jana Nina hakika utakuwa umeangalia ni vipengele gani vya kimaisha ambavyo vitakuwa vumekutokea huku vikiwa kama majaribio kwako.

Kama hukusoma Makala ya Jana bonyeza hapa uisome kabla ya kuendelea

maisha kama makabidhiano
Kila kitu ambacho unacho hapa duniani umepewa kwa muda tu! Hakuna kitu ambacho unakimiliki wewe kama wewe hivyo unahitaji kukitumia vizuri ukijua kwamba mwisho wa siku utatakiwa kutoa hesabu ya kile ulichopewa. (Kwa lugha nyingine utatakiwa kutoa maelezo ya jinsi ulivyotumia zawadi ulizokabidhiwa).

Muda ulio nao umekabidhiwa, hivyo unahitaji kuutumia vizuri

Mahusiano yako unahitaji kuyataunza maana nayo umekabidhiwa kwa muda tu.

Marafiki wako ishi nao vizuri maana nao umekabidhiwa tu.

Mke au Mme wako umekabidhiwa hivyo mpende.

Vipo vitu vingi ambavyo umekabidhiwa na unapaswa kuvitumia. Vitu hivi ni kama akili, nguvu, ardhi, watu kutaja ila vichache.

Kuna vitu watu wamekabidhiwa ila hawajui kama wanavyo. Yaani unaqeza kupita katikaasha unatambaa, wakati wewe hukutakiwa kuwa unatambaa badala yake ulipaswa kuwa unakimbia. Hii ni kutokana na kwamba watu hawataki kujua vitu walivyokabihiwa ni vipi na wavitumie kwa namna gani?

 Kuna hadithi ya bwana mmoja Wa ajabu aliyekuwa na nguvu za ajabu. Alikuwa anaweza kumfanya kila mtu jinsi ambavyo anataka. Siku moja alikaa na kujiuliza hii nguvu yote nitaiweka wapi?

Ndipo mshauri wake mmoja akamwambia kwamba akaiweke mlimani. Mshauri huyo akaendelea kusema, “endapo utaiweka huko basi hakuna atayeiona”

Lakini yule bwana akasema binadamu wanaweza kupanda mpaka kule na kuiona.

Mshauri Wa pili akapendekeza aiweke baharini. Akasisitiza kwamba hakuna atakayeweza kuiona.

Lakini yule bwana akasema binadamu wanaweza kuogelea na kufika huko, mwisho Wa siku ikachukuliwa na binadamu mmoja tu.

baada ya kufikiri sana. Alisema “tuiweke kwenye mioyo na akili za binadamu maana wao ni wazembe, hawataweza kuiona”

Kumbe kuna kitu umekabihiwa hapo ulipo na unapaswa kukifanyia kazi.

Ili tuweze kuelewa vizuri sana juu ya somo hili la makabidhiano naomba tuuangalie mfano huu.

Familia moja ilienda kutembea katika mji mmoja mkubwa hapa nchini. Wakiwa huko rafiki mmoja wa familia hiyo aliwapa nyumba ya vyumba vinne, yenye kila kitu. Ikiwemo bustani, swimming pool, vitanda na kila kitu.

Rafiki yule aliiambia familia ile, “tumieni vitu hivi kama vile ni vya kwenu”.

Hivyo familia ilifurahia maisha ikiwa kwenye ile. Watoto walijirusha kwenye vitanda kama vile wapo nyumbani, walicheza michezo kadha wa kadha ya kujificha.

Hali kadhalika wazazi walijiachia. Mme na mke wake walikuwa nao wakifurahia maisha chumbani kwao.

Ila kwa wakati wote waliokuwepo pale baba alihakikisha kwamba ile nyumba wanaiweka katika hali ya usalama maana pake walikuwa wamekabidhiwa kwa muda tu

Hali kama hii ndio inajitokeza kwenye uhalisia wa maisha.

Maisha ni makabidhiano. Ila hakikisha unatumia haswa kile ambacho umekabidhiwa kabla kukirudisha ili mwisho Wa siku unapokirudisha yule aliyekukabidhi anafurahi na anapenda akupatie zaidi. Usikuabali kuacha kitu jinsi kilivyo.

Hakuna mtu makini ambaye atakukabidhi kitu akapenda kukuta umeharibu. Kila mtu anapenda akute umeendeleza kitu kile ulichokabidhiwa. Umefanya kwa namna ya tofauti.

Katika kurasa za Biblia tunakutana na hadithi ya mfanyabiashara mmoja ambaye alipotaka kwenda nchi ya mbali, aliwaita watumwa wake watatu. Mmoja akamkabidhi talanta tano, mwingine talanta tatu, ma mwingine alimkabidhi talanta moja.

Yule aliyekabidhiwa talanta tano alifanya nazo Biashara na kupata tano zaidi.

Yule aliyepewa Tatu naye alifanya Nazo Biashara na kupata Tatu zaidi.

Lakini yule aliyekabidhiwa moja, aliichimbia chini ili isionekane.

Yule bwana aliporudi (mfanyabiashara) alitaka kupata hesabu ya kile alichokuwa amewakabidhi.

Aliyekuwa amekabidhiwa talanta tano, alitoa hesabu zake na talanta zaidi. Hali kadahalika mwenye talanta tatu. Lakini yule mwenye talanta moja aliishia kusema “ _nalijua kwamba wewe ni mtu mgumu, unavuna usipopanda, hivyo niliificha, sasa chukua kilicho chako_”

Yule bwana  (mfanyabiashara) hakupendezwa na mtumwa huyu ambaye hakuweza kuitumia vizuri talanta yake hii moja.

Je, na wewe ni mmoja wao? Unaitumia kweli talanta yako ukiyokabidhiwa? Kumbuka kwamba maisha haya ni makabidhiano. Umekabidhiwa ila usiache vitu kama vilivyo.

Ukishindwa kuviendeleza utanyangwa na watapewa wengine wenye uwezo wa kuviendeleza zaidi.

Hali kama hii naona haikumtokea yule bwana tu. Ila hata hapa tunapoishi duniani. Kuna watu wanakabidhiwa vitu na kuambiwa waviangalie, wakishindwa wanatolewa au kunyang’anywa.

Katika kijiji ninapoishi unaweza kununua mfugo wako na kumkabidhi jirani au Rafiki yako ambaye unajua atautunza. Hali hii nimekuwa naiona nikiwa Mdogo mpaka leo hii ninapoandika makala haya. Ila kama ukiyemkabidhi haoneshi hali ya kuujali mfugo wako basi kumnyang’anya kunahusika.

Kuwa makini usije kunyanga’anywa ulichokabidhiwa maana maisha haya ni makabidhiano.

Na
Coach Godius Rweyongeza
Mwandishi
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X