Ukipambana Na Nguruwe Utachafuka Mwenyewe Lakini Yeye Atafurahia


kila siku kuna mambo mapya ambayo yanatokea kila siku. unahitaji kupambana kila siku katika safari yako yako ya kuhakikisaha kwamba unataka kufikia kileleni. unahitaji upambane kwa kwa ujasiri wa hali ya juu sana. kuapambana ni sifa moja kubwa sana ambayo wajasiriamali wanayao. hii ni sifa, ambayo inawatofautisha wao na watu wengine, ambao wana maisha ya chini sana.

Katika makala ya leo kuna mtu mmoja ambaye nataka kukwambia kwamba huyu mtu huhitaji kupambana naye wala kupoteza muda wako ukiwa naye. maana kwa kufanya hivyo utajikuta ukipoteza muda mwingi sana ambao ungekuwa nao kwa ajili yako kufanya shughuli nyingine nyingi sana,

Je unamjua mtu huyu ni mtu gani? huyu ni mtu ambaye anakukatisha tamaa na kukurudisha nyuma. uusipoteze muda wako hata kidogo kwa kubisha naye wala kuongea naye ukijaribu kumshawishi iili aaweze kuendana na wewe. utapoteza sana muda wako. muda wako wa kufanya mambo makubwa ni leo waache wale ambao wanaongea ili wakukatishe tamaa waongee lakini usipoteze muda wako kubisahana nao.

kuna msemo mmoja ambao unasema kwamba ukipambana na nguruwe utapoteza utachafuka wewe mwenyewe lakini yeye atafurahia hali hiyo. Ukipambana na mtu ambaye hajielewi utakuwa unapoteza muda wako, ukipambana na mtu ambaye haoni umuhimu wako na kutaka kumweleza au kumwonesha ubora ambao wewe unao utakuwa unapoteza muda wako. Hii ni sawa na kupambana na nguruwe , wakati yeye anafurahia matope wewe utakuwa unachafuka.

Sio lazima kila mbwa ambaye anakubwekea umkemee ni methali ya kenya. sio lazima kila mtu anayekuvuta uangukie upande wake, sio lazima kila mziki unaochezwa wewe uucheze. ni uamuzi wako kuucheza au kuuacha. chukua hatua sasa.


One response to “Ukipambana Na Nguruwe Utachafuka Mwenyewe Lakini Yeye Atafurahia”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X