Usidanganyike Maisha Bado Yanaendelea


habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa makala za songa mbele. imani yangu siku ya leo umeianza kwa namna ya tofauti kabisa. karibu sana katika makala ya leo ambapo tunaenda kujifunza kitu kipya ambacho hatujawahi kujifunza maishani mwetu. 

bila shaka jana uliweza kufanya kitu kikubwa sana jana ambacho mpaka leo hii unashangilia ushindi wake. Nichukue nafasi hii kukupongeza ka ushindi mkubwa sana ambao ulipata kwa siku ya jana, lakini  kumbuka kwamba leo ni siku nyingine ya tofauti na mapambano bado yanaendelea. kumbuka kwamba leo hii unapaswa kufanya kitu cha tofauti na kuendelea kuweka alama katika dunia hii.

kumbe usidanganyike na mafanikio ya siku ya jana maana leo ni siku nyingine ya tofauti sana.

usiseme kwamba jana nilisoma sana vitabu! bali siku ya leo inapaswa kuwa ya tofauti kabisa na siku nyingine zote. jana haipaswi kuwa bora zaidi ya leo. Kwa sababu leo ni siku ya kipekee sana. ukiona jana imekuwa bora zaidi ya leo jua kwamba kuna sehemu umedanganyika na hujaishi kwa namna ambayo ulipaswa kuishi. ishi leo hii rafiki yangu ili uweze kufikia hatua kubwa sana ya kimafanikio. LEO NI LEO ASEMAYE KESHO NI MWONGO.

Usiseme kwamba nilichokipata kinatosha. maana kadri utakavyozidi kusema kwamba inatosha utashangaa hata kile ulicho nacho unazidi kukipoteza. kumbuka kwamba huwa ni rahisi sana kwa mwanafunzi kutoka A kwenda F kuliko wanafunzi kutoka F kuja A. Pigana leo hii kuhakikisha kwamba unalinda heshima yako. Fanya kile ambacho unapaswa kufanya siku ya leo, kifanye kwa namna ya utaoauti sana.

 kuwa na siku njema sana.
kuwa na safari njema sana ya kuhakikisha kwamba unaweza kukifikia kilele ambacho ndilo jukumu  la kila mmoja wetu.

 

Endelea kusoma makala za kuelimisha na. Kuhamasisha  kutoka kwenye blogu hii

Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X