Dunia ya sasa inazidi kukua kwa kasi kubwa sana. Kadri dunia inavyozidi kukua kutangaza Biashara kunakuwa rahisi lakini pia kunakuwa kugumu. Wale wanaobadilika na wakati wanaweza kutangaza boashara zao na kuwafikia wateja wengi. Wale wanaokomaa na njia zile zile za jana basi wanazidi kupitwa. Ili kukurahisia njia za kuitangaza Biashara yako basi hapa nimekurahisishia. Kiufupi ni kwamba nimekuandalia njia za kuitangaza biashara katika dunia ya sasa.
1. Matangazo redioni
2. Kufanya matangazo mwanzoni mwa filamu.
3. Kufanya mahojiano kwenye televisheni
4. Kutangaza bidhaa zako kwenye magazeti, majarida na vipeperushi
5. Mahojiano redioni.
6. Kuandika makala kwenye magazeti.
7. Kwa kuandaa vidio fupi fupi za kuitangaza bidaa yako.
8. Matangazo ya redioni
9. Kwa kutumia blogu yako
10. kwa kutumia blogu ya rafiki yako.
11. Kwa kuwaomba watu wakutangaze kupitia maandishi yao
12. Kwa kutumia sehemu ya kuweka status ya wasapu
Soma zaidi; Mambo Ya Kuzingatia Ili Kuchagua Fursa Sahihi
13. Kwa kutumia sehemu ya kuweka profile picture Facebook, waspu na mitandao mingine.
14. Kwa kuitumia mitandao ya kijamii
15. Shiriki kwenye semina na mikutano ya kibiashara
16. Kwa kutumia email za watu.
17. Kwa kutumia namba za simu za watu. Kuwapigia au kuwatumia jumbe fupi au SMS.
18. Kwa kutoa semina ya bure au ya malipo.
19. Mapambo kwenye uwanja wa mpira.
20. Mabango mbali mbali kwenye miji.
21. Matangazo ya maandishi kwenye magari
22. Kwenye makongamano na warsha zinazojitokeza kwenye jamii yako.
23. Kwa kudhamini mashindano ya michezo eneo ulipo.
24. Tengeneza tisheti, kofia, mabegi, viatu n.k
25. Weka matangazo kwenye maduka au majengo ya makampuni makubwa
26. Ongea na watu moja kwa moja.
27. Fanya maonesho ya bidhaa yako.
28. Kuwa na mabalozi wa bidhaa yako sehemu mbali mbali.
29. Tangaza kwa kupunguza bei
30. Tangaza kwa kuwatembelea wafungwa, walemavu wagonjwa n.k
31. Itumie vizuri sehemu ya MAUZO kwenye ukurasa wako wa Facebook page na makundi ya facebook,
Chagua njia ambazo unaona zinakufaa kwa ajili ya wewe kuzitumia. Chagua ambazo unaona ni bora kwako.