Iko Wapi Sehemu Tajiri Duniani Ili Nikatengeneze Pesa?


Kumekuwa na wimbi la vijana kuhama kutoka vijijini kwenda mijini ili wakatafute pesa. Wanatafuta sehemu ambayo itakuwa njema sana kwa ajili ya mafanikio yao.

Je, wakifika mjini wanafanikiwa?
Wapo ambao wanafanikiwa, mara tu baada ya kufika mjini na wapo ambao bado maisha yanazidi kuwa magumu. Sasa zile ndoto za twende mjini kuna maisha mazuri zinaaanza kupungua na kukuta watu wanapoteza mwelekeo.

Sasa iko wapi sehemu tajiri ili mimi niende nikatengeneze pesa? Nani anaweza kuniambia sehemu ambapo mimi Godius Rweyongeza nikizaliwa jumatatu,
Nikaenda kule jumanne
Jumatano nifanye kazi
 Alhamisi niwe tajiri?

Iko wapi sehemu ya aina hii!?
Nani anaweza kuniambia sehemu hii iko nchi gani?

Je, ni kwenye machimbo ya migodi Arusha, Geita, au Kahama?

Je, ni kwenye Kilimo cha mpunga Morogoro?.

Au ni Kilimo cha Kahawa mkoani Kagera na Mbeya?

Au inawezekana ikawa ni kule Mikumi, Kilimanjaro na Zanzibar kwenye utalii?

Ni wapi sasa ambapo naweza kuwa utajiri wa haraka ndani wiko moja?

Haya ni maswali ambayo watu wengi (wakubwa kwa wadogo). Ambao wamefikia umri wa kuijua pesa. Wanajiuliza kila siku.

Katika makala hii kuna jibu la wapi kuna unaweza kuukuta utajiri wa haraka.

Sehemu pekee ambapo kuna utajiri wa kila aina. Ni makaburini?

Hee! Naona unashangaa! Ulitegemea nishushe dili la pesa hapa fasta. Sasa nimekuchanganya. Ebu endelea kusoma kidogo.

Makaburini kuna watu ambao walikuwa na mawazo makubwa sana ila hata hawakuwahi kuchukua hatua. Kuna watu walikuwa na vipaji vikubwa sana ndani yao ila hawakuwahi kuchukua hatua. Leo hii wapo makaburini wamelala. Hakika mle kuna utajiri mkubwa kuliko utajiri ambao upo sehemu kwenye migodi ya madini ya dhahabu.

Soma zaidi; Hii Ni Barabara Ambayo Unaweza Kuichukua Maishani

SASA HII INA MAANA GANI?
Kama makaburini ndipo kuna watu wenye utajiri mkubwa sana, utanisaidiane Mimi kutajirika?

Hii ni muhimu sana kwako? Yaani kama kuna watu ambao wamekufa na utajiri mkubwa. Kama kuna watu wamekufa na vipaji ndani yao, basi na wewe chukua hatua! Usife na ile nguvu ya kufanya vitu ambayo imo ndani yako.

Kuna dhahabu kubwa sana ndani yako? Hakikisha kwamba unagundua dhahabu hii na unaitumia.
Dhahabu hii ipo  kwenye kusudi lako na vipaji vilivyoko ndani yako.

Haya hapa maswali muhimu ya kukusaidia kujua kusudi na kipaji chako!

Mimi ni nani?
Kwa nini Niko hapa?
Je, naweza kufanya nini?
Kitu gani naweza kufanya kwa ubora zaidi ya watu wengine?
Kitu gani ambacho kama sitakuwepo hakifanyiki vizuri?
Nifanyeje ili niongeze uwezo wangu?

Hakika ukiyajibu maswali haya vizuri utakuwa umeanza kupiga hata kuelekea mafanikio!

Na kama utagundua kwamba makaburini ndipo kuna utajiri mkubwa sana, na utajiri ule umewekwa na watu. Basi utajiri mkubwa utakuwa ndani yako. Basi kiufupi niseme kwamba sehemu tajiri kuliko zote ni ndani yako.  Utumie utajiri huu. Kwa manufaa ya watu wengine na wewe mwenyewe…

Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com

Ili kupata kitabu cha kutokaa sifuri mpaka kileleni tuwasiliane 0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X