KITU HIKI KITAKUNYIMA KAZI KAMA KWA SASA UNATEMBEA NA CHETI


Habari za siku ya leo rafiki yangu, imani yangu kwamba siku ya leo ni njema sana na mambo yako yanaenda vizuri sana.   kama kuna kitu ambacho unataka kufanya leo hakikisha kwamba unakifanya kwa ajili ya baadae.  Hakikisha kwamba kile ambacho unataka kukifanya ndani ya siku hii ya leo unakifanya tena uhakifanya kwa juhudi kubwa sana.

leo hii nimeamua kuongea na wale ambao bado wapo mtaani wanatembea na vyeti wakitafuta ajira. kuna kitu kimoja ambacho mnakifanya ambacho hakitakuja kuwapa ajira. ndio yawezekana kwamba kazi ipo lakini hiki kitu ambacho unakifanya leo hii ndicho kitu ambacho kitakuja kukunyima ajira kabisa.

hasa hii inakuhusu wewe mwanadada, au wewe mzazi ambaye una mtoto wako wa kike. yawezekna haufanyi wewe lakini hakikisha kwamba unamtahadharisha sana mtoto wako ili asije akafanya kosa hili. maana litakuja kumgharimu sana. kosa hili litahatarisha sana maisha yake. Hakikisha kama ni wewe ni mdada haufanyi kosa hili. maana linaweza kuwa la hatari sana kwenye maisha yako.

Soma zaidi;  Hii Ndio Siri Iliyonyuma Ya Kuwa Updated

ndio ni la hatari sana. kosa lenyewe ni kujirahisisha. ndio rahisi kama hivyo lakini ikiwa na maana kubwa sana. kama unatafuta kazi na unazunguka na cheti hakiksha kwamba haujirahisishi na kuonesha kwamba wewe upo tayari kumpa mtu atakayekupa kazi  chochote kile ilimradi upate kazi. hii sio kiki nzuri ya kuingilia wakati wa kutafuta kazi. hii ni hatari sana kwa afya yako, lakini pia kwa ajiri ya future yako. mwili wako ni kitu muhimu sana ambacho unapaswa kuhakikisha kwamba unakilinda kwa ajili ya siku zako za mbeleni. kama unaona kujirahisisha ni njia nzuri sana ya wewe kuendelea kuishi hapa mjini. sichelei kusema kwamba umekosea sana. hakikisha kwamba unatafuta maarifa mengine ambayo yanaweza kukusaidia wewe kuweza kupata maisha mengine bora zaidi.

sio lazima uingie ndani ya ajira. kwa maana mpaka unaanza kuzunguka na cheti mtaani, jua kwamba una kitu kichwani mwako ambacho unaweza kukitumia kwa kuanzia na kuhakikisha unaweza kutoka hapo ulipo na kwenda hatua ya ziada. usijirahishe hata kidogo. tumia ujuzi mdogo ambao umejifunza shuleni kwa kuanza kujiajiri.

Ndimi
Kocha Godius Rweyongeza
0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X