Habari,
Namshukuru Mungu kwa siku hii njema sana ya leo.
Watu wengi sana wamekuwa wakiuliza ipi biashara bora wao kufanya. Na mara nyingi sana watu wamekuwa wakishabikia fursa mbali mbali ambazo zinajitokeza.
Mwaka unapitia katika vipindi vingi sana. Ambapo ndani ya mwaka husika huwa zinajitokeza fursa mbali mbali. Zipo fursa ambazo huwa zinajitokeza kwa muda mfupi. Na zipo fursa ambazo huwa zipo januari mpaka disemba. Na kuna fursa zinazosemekana kuwa ni za nyakati zote.
Mfano katika biblia kuna mtu anaitwa Ibrahim ambaye alikuwa mfanya biashara maarufu sana? Je, ulikuwa unajua hili? Kama ulikuwa hujui Ibrahimu alifanya biashara na alizitumia fursa au biashara za wakati huo. Miongoni mwa biashara alizozifanya zilikuwa hizi hapa;
>>Trading
>>real estate
Hii ni kusema kwamba fursa zimekuwepo tangu zamani sana. Hata sasa hivi ninapoongea kuna fursa zilizogeuzwa kuwa biashara kipindi hicho na mpaka sasa hivi bado zinageuzwa kuwa biashara.
Lakini pia kuna fursa za muda mfupi ambazo huwa zinajitokeza mwanzoni, katikati au mwishoni mwa mwaka.
Kuna fursa ambazo huwa zinatokeza kwenye maeneo kwa msimu. kuna fursa ambazo huwa zinajitokeza mara moja kwa mwaka, baada ya miaka miwili, baada ya miaka mitatu, minne n.k
Mfano wa fursa ambazo huwa zinajitokeza kwa msimu ni fiesta, kombe la dunia, uchaguzi n.k
Sasa kwa siku ya leo tuangalie mambo ya kuzingatia wakati wa kuangalia fursa sahihi kwako!
1. Utayari.
Jambo la muhimu sana katika kujenga biashara bora ni utayari wako. Maana siku zote kujenga biashara yenye mafanikio kunaanzia kwako. Hakikisha kwamba unajijenga kifikra! Hakikisha kwamba upo tayari kuchukua hatua kuanza kukuza na kujenga biashara yako.
>>> una uwezo wa kumudu hatari?
>>>umejiandaa kupambana na changamoto za kibiashara
>>>ni upi mtazamo wako juu ya kufanya makosa katika biashara na maisha?
>>>Unahitaji kuwa tajiri au unatamani kuwa tajiri?
Soma zaidi;Usidanganyike Maisha Bado Yanaendelea
2. Je, unajua pesa zinapopatikana?
Kabla ya kwenda mbali na uwekezaji lazima ugundue pesa zilipojificha. Pesa zipo sehemu mbali mbali kama vile.
>>>kwa watu
>>>kwenye matatizo
>>>kwenye huduma
>>>kwenye ndoto
>>>kwenye mawazo
>>>kwenye mawazo
>>>kwenye kazi (shughuli)
>>>kwenye mbegu (upande wa kilimo)
3. Una mtaji kiasi gani?
Mtaji ulionao ni kigezo kingine ili uweze kuchagua fursa ipi uifanyie kazi. Fursa ya kuchagua kwa mtu mwenye laki tano ni inaweza kuwa na tofauti na milioni 20.
4. Upo mwenyewe au una timu ya watu?
Lazima ujue kama unafanya mwenyewe au utahitaji watu wa kufanya nao kazi. Hii itakusaidia kujua fursa ipi unapaswa kuchagua na uingie katika biashara.
Kuna biashara huwezi kufanya mwenyewe unahitaji wasaidizi.
5. Mpango wako wa biashara ukoje?
Ukiwa na mpango wa biashara mzuri, timu nzuri na utayari kifikra basi unaweza fanya makubwa kwenye dunia hii iliyojaa fursa kila kona.
Kwa leo hii tunaishia hapo. Wiki ijayo tutaendelea na vitu vingine muhimu vya kuzingatia katika kuchagua fursa.
Endelea kufautilia na kusoma makala mbali mbali kutoka katika blogu hii.
Ndimi rafiko na ndugu yako
Kocha Godius Rweyongeza
0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com
Asante
Umekuwa nami,
GODIUS RWEYONGEZA
Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA
Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA
Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA
Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391
kila la kheri