Mambo Ya kuzingatia Ili kuchagua Fursa Sahihi


Habari wiki iliyopita, tulianza kuzungumzia juu ya mada inayohusu mambo ya kuzingatia ili kichagua fursa sahihi. Leo hii tunaendelea na mada hii ikiwa ni sehmu ya pili na hapa tunaenda kumalizia mambo mengine matano ya kuzingatia ili kuchagua fursa sahihi. Hakikisha kwamba umesoma kwanza makala ya wiki iliyopita kwa kubonyeza hapa; baada ya hapo unaqeza kuendelea kusoma makala ya leo.

6. Una wazo gani la biashara kichwani?
Wazo bora la biashara hutofautiana kutoka kwa mjasiliamali mmoja na mwingine kulingana na falsafa na mazingira yanayowazunguka. Wazo lako litatofautiana na langu kulingana na vitu mbali mbali ikiwemo eneo ulilopo, shauku yako, kile ukipendacho, ujuzi, jiografia, ardhi ya eneo, mahitaji ya watu, usambazi, sera za kiuchumi na mengine mengi.

7. Je, unaweza kuuza bidhaa.
Je, una uwezo wa kukutana na watu na kuwashirikisha juu ya bidhaa yako uliyo nayo. Kama hujui kuuza ni bora ukachukua bidhaa ndogo ndogo na kuanza kuuza. Hii itakusaidia kuzijua na kujipanga ni kwa jinsi gani inaweza kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kwenye uuzaji. Nakumbuka Robert Kiyosaki katika kitabubchake Cha Before You Quit Your Job anasema  kwamba “alijiandikisha kwenye mafunzo ya uuzaji na alianza kuuza bidhaa muda wake wa ziada wa usiku”.  Hivyo na wewe unaweza kufanya hivi ili pale utakapoamua kuanza rasmi biashara walau uwe na ujuzi kidogo juu ya masuala hayo ya uuzaji.

Kumbuka kwenye kuuza bidhaa unapaswa kuwa mnyenyekevu, mvumilivu, kauli nzuri kwa wateja na, heshima na nidhamu, jitihada na juhudi, msafi wa mwili na mavazi (hasa kwa biashara zinazohisisha vyakula), kujiamini na uwe mtu unayejua kwenda na muda.

8. Je, unatafuta nini kwenye biashara?
Kuna watu hawajui kwa nini wanafanya biashara? Yaani wao wanafanya ilimradi tu wamepata pesa kidogo ya kuufanya mdomo uingie kinywani. Hii ni hatari sana ndio maana watu walio wengi huwa wanapoteza motisha ya kibiashara.

Soma zaidi; Iko wapi Motisha Ya Januari Mosi

Ukiwa na lengo dogo la kibiashara kamwe biashara yako haiwezi kukua.

Moja kati ya makala ambazo amewahi kuandika mwandishi Edius Katamugora ni makala yake ya septemba, 13. Anasema “kama unataka kuwa almasi lazima uwe na sababu 10 za kwa nini uwe almasi”.  Sasa huu ndio muda wako wa kujiuliza kama unataka kuwa mfanya biashara maarufu ziko wapi sababu kumi za kunifanya kiwa mfanya biashara maarufu?
Chukua hatua!

9. Je, unazijua kanuni za pesa?
Kila kiti kina kanuni zake? Huwa napenda kuwaambia marafiki wangu kwamba mtu akitaka niitawale dunia basi aniambie tu kanuni za kuitawala, inatosha. Maana ukizijua kanuni za kitu maisha yanakuwa rahisi sana. Ukizijua kanuni za mpira wa miguu lazima utaupenda tu mpira wa miguu.

Hivyo hivyo ukizijua kanuni za pesa zitakusaidia kufanya biashara.

Soma zaidi pesa nini?

>>> peaa ipo kukufanyia wewe kazi sio wewe kufanyia kazi pesa.
>>> pesa inabidi itawaliwe sio yenyewe itawale
>>> watu ndio wanapaswa kuwa kipaumbele na huduma unazotoa zinapaswa kulenga watu na pesa zitafuata.

>>> pesa itunze na itumike kufanya jambo la msingi sana. Si kila kitu ambacho unaona machoni pako lazima ukifanye. Hii si kweli. Lazima ujifunze kutumia pesa kwa matumizi sahihi.

Ndimi
Kocha Godius Rweyongeza
0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X