Maswali Muhimu Unayopaswa Kujiuliza Kila Unapoamka Asubuhi


Je, kitu gani unafanya unapoamka asubuhi?
Je, unasoma Malengo yako?
Je, unasoma Kitabu?
Je, Unakimbilia kushika simu ili uangalie kitu gani kinaendelea mtandaoni?
Unawahi kuangalia picha yako uliyopost Jana ina likes ngapi?
Unawahi kuangalia comment yako kwenye picha ya Rafiki, kuangalia amekujibu nini?
Unafanya nini kikiwa cha kwanza asubuhi?
Je, unaanza kufikiri Kile ambacho hukufanya vizuri jana? Pole sana, ila kumbula ya jana yamepita ndio maaana tumekufa kwa kulala, sasa tumeamka ili tuzidi kusonga mbele. Ya Jana hayana maana tena!
Sasa unafanya nini?
Au labda unafikiri juu ya Biashara au mpenzi uliyempoteza Jana.
Labda unafikiri juu ya yule mwalimu aliyekwambia usipomaliza kazi leo atakuchapa!
Labda unafikiri maisha ni magumu!
Mimi sijui.
Ila ninachojua ni kwamba kuna maswali ya muhimu sana ambayo unapaswa kuwa unajiuliza kila unapoamka asubuh. 
Maswali haya utapaswa ujiulize mara tu baada ya  kusoma malengo yako.
Ni maswali muhimu ambayo pia unaweza kujiuliza katikati mwa siku.
Chukua kalamu na karatasi sasa uanze kujibu swali moja baada ya jingine.
1. Je, ninafanya nini ili kuibadilisha leo!
2. Je, nawezaje kuwa wa thamani kwenye jamii hii iliyonizunguka?
3. Je, nawezaje kuongeza huduma yangu leo?
4. Je, muda wa kuendesha Biashara yangu nitautoa wapi siku ya leo?
5. Je, ni majukumu gani nitayafanya mimi siku hii ya leo na ni majukumu gani yatafanywa na watu wengine?
7. Je, ni vitu gani vitatu muhimu leo  nitaweza kuvifanya kwa ubora?
8. Nitawezaje kuongeza Maarifa yangu siku ya leo?
Hayo ndio maswali muhimu unayopaswa kujiuliza kila unapoamka asubuh.
Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
Songambele
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
www.songambeleblog.blogspot.com
Vitabu muhimu vya kusoma ili uongeze wigo wako wa Maarifa.
1. Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni By Godius Rweyongeza
2. Lead The Field By Earl Ninghtngale
3. The Secret Of A Millionaires Mind by T.Harv Eker


One response to “Maswali Muhimu Unayopaswa Kujiuliza Kila Unapoamka Asubuhi”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X