Nafasi Muhimu za Watu Katika Biashara.


Ili biashara yoyote iweze kukua inahitaji timu ya watu ambao wataungana kuhakikisha kwamba wanaikuza. Mtu mmoja hawezi kuikuza Biashara na kuifanya iwe yenye manufaa makubwa.

Kumbe ndio maaana suala zima la mahusiano mazuri kati ya mmiliki wa biashara na wafanyakazi wake ni muhimu.
Huhitaji kuanzisha Biashara ukiwa unajua kila kitu. Unahitaji kuwa kiongozi mzuri ili uweze kuiunganisha timu yako ya Biashara.

Kumbuka kila mtu katika Biashara yako ana namna tofauti ya kufikiri, kipaji, ujuzi, kutenda, kisomo,n.k

Ukiweza kuunganisha vitu hivi, utakuwa umejihakikishia ushindi mkubwa katika Biashara.

Je, wewe ni mfanyabiashara?
Je, wewe umeajiriwa katika Biashara fulani?
Je, umejiajiri?

Je, unaifahamu nafasi yako katika biashara unayofanya?

Soma zaidi; Iko Wapi Motisha Ya Januari Mosi?

Kuna nafasi muhimu ambayo tunategemea kila aliye katika Biashara husika ataangukia. Nafasi hizi zinaweza kuchukuliwa na meneja, mhasibu, au mtu yeyote katika kazi!
Nafasi zenyewe ni

1. Nafasi ya wataalamu.
Mara nyingi hawa ni watu qaliomaliza shule (hasa chuo) na kuna ujuzi fulani  wanao. Ni kupitia ujuzi huu kwamba wanafanya kazi katika biashara husika.
Watu hawa ni kama wahasibu, madaktari, wahandisi, n.k

2. Nafasi ya uongozi.
Hawa ni watu ambao wanashughulika na miongozo ya kampuni na kuhakikisha kwamba kampuni imekua kwa kwa kuweka Sera nzuri na kuhakikisha zinatekelezwa.
Mfano wa watu hawa ni meneja, mkurugenzi, wakuu wa idara mbali mbali lakini hata sekretari.

3. Watu mauzo.
Hawa ndio wanajenga msingi mkubwa wa kuhakikisha kwamba kampuni linaendelea kupumua. Watu hawa ndio wanahakikisha kila bidhaa inayozalishwa na kampuni husika inauzwa. Watu hawa ndio moyo wa kampuni.
Wanaweza kuwa wamesomea mauzo vyuo au hawajasomea kabisa ila wana ujuzi huo.

Je, wewe ni nani?
Je, unawafamu watu hawa muhimu kwenye Biashara yako?
Kama umeajiriwa unaifahamu nafasi yako?

Chukua hatua sasa.

Ndimi
Kocha Godius Rweyongeza
0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com
Aaante


Ndimi rafiki na ndugu yako

Kocha Godius Rweyongeza
0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com
Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa watu maalumu kwa kubonyeza hapa


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X