Nchi Za Ulimwengu Wa Tatu? Au Watu Wa Ulimwengu Wa Tatu? Ipi Sahihi?


Kumekuwa na hali ya watu kuambiwa kwamba wao ni wazembe. Kwamba hawawezi na wao wanakubali. Hakuna aliyezaliwa akiwa wa kawaida sana kama ambavyo jamii yako inakuona. Wewe ni zaidi ya hapo.

Jamii inamuona mtu aliye gerezani kama mfugwa lakini. Kama na yeye atajiona mfugwa basi maisha yake yote atakuwa mfugwa tu. Lakini kama atajiona  kama mwanamziki maarufu, raisi wa nchi au mwandishi wa kitabu maarufu, ataweza kuwa.
Nelson Mandela alifungwa miaka 27 gerezani. Siku zote hizo hakuwahi kujiona kama mfugwa bali kama mkombozi na mtetezi wa haki za binadamu.

Kumbe hapo ndipo ukweli wa maneno ya kwamba “jamii inapokupa limau wewe tengeneza sharubati” unajitokeza.

Kuna watu wameaminishwa kwamba kuna nchi za ulimwengu wa tatu. Huku wakizitolea tafsiri nchi hizi kwamba ni nchi maskini, nchi zilizonyuma kiteknolojia na nchi zilizonyuma kiuchumi.

Kwa maoni yangu nchi za ukimwengu wa tatu hazipo. Wala hazijawahi kuwepo. Ila kuna watu wa  ulimwengu wa tatu.

Watu wa ulimwengu wa tatu wapo duniani kote. Marekani kuna watu watu wa ulimwengu wa tatu. Urusi kuna watu wa ulimwengu wa tatu. Afrika kuna watu wa ulimwengu wa tatu. Amerika kusini kuna watu wa ulimwengu wa Tatu.
Haijalishi mtu Huyu kaenda mwezini au la! Haijalishi mtu huyu kapanda ndege na wewe hujapanda kama ni mtu wa ulimwengu wa tatu atabaki kuwa wa ulimwengu wa tatu  mpaka pale atakapobadilika.

Pata nakala ya kitabu hiki sasa hivi kwa kulipia tsh. 5000. Bei hii ni ya punguzo (kuanzia tarehe 25 septemba mpaka tarehe mosi oktoba). Baada ya hapo kitauzwa kwa bei ya 10000. Chukua hatua sasa.

Watu wa ulimwengu wa tatu ndio akina nani?
Hii hapa ndio orodha sahihi ya watu wa ulimwengu wa tatu.

1. Ni watu wanaokubali kwamba wao ni wa kawaida wakati wao si wa kawaida. Wala hawakuzaliwa wakiwa wa kawaida.

2. Ni watu wanaokubali maoni ya watu wengine na kuupoteza ukubwa uliondani yao.

3. Watu wanaokubali kwamba wanayumba yumba wakati wao ni miti imara.

4. Watu wanaokubali kuitwa jani wakati wao ni miamba.

5. Ni watu ambao hawajui wanapaswa kufanya nini! Wanasubiri waambiwe na rafiki zao au viongozi kwamba sasa kafanye hiki. Wanasubiri waambiwe kwamba acha hiki.

6. Watu wasiokuwa nanmalengo. Watu wasiojua leo wanapaswa kufanya nini.

Hawa ndio watu wa ulimwengu wa tatu. Wapo kila nchi.

Nchi yetu itakuwa juu, tena juu sana. Kama watu wa ulimwengu wa tatu watapungua.

Tukianza kuona jicho la dhahabu ndani yetu sisi wenyewe. Na mtu wa kwanza kujiona wa thamani ni wewe mwenyewe. Hawa wengine watajazia tu.

Mtu wa kwanza kuona kiwanda kikubwa kimejengwa ni wewe. Vitu vingine ni mbwembwe tu..

Chukua hagua sasa. Wewe ni zaidi ya ulivyo sasa.

Jipatie sasa kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI. kwa bei ya punguzo. Yaani punguzo la asilimia hamsini. Kitabu hiki kwa sasa (kuanzia tarehe 25 septemba mpaka tarehe 01 oktoba) kinapatikana kwa pesa za kitanzania 5000.
Lipa pesa yako kwenda namba 0755848391 sasa ili ujipatie kitabu hiki.

Kitabu hiki kipo katika mfumo wa nakala tete (soft copy) na kinatumwa kwa njia ya email popote pale ulipo duniani.

Baada ya kufanya malipo yako nitumie ujumbe wasapu kwenda namba 0755848391 wenye email yako. Utapokea kitabu chako dakika chache baada ya kutuma pesa yako. Karibu sana.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X