TATIZO SI RASLIMALI ZILIZOPOTEA -7


Thamani ya yako si kama thamani ya nguo. Thamani yako si kama thamani ya nyumba au gari lolote unalolifahamu.

Wewe unayo thamani kubwa, kubwa, kubwa sana. Thamani yako imo ndani yako tangu siku ulipozaliwa. Ni thamani kubwa sana.

Tofauti ya thamani kubwa iliyo ndani yako na thamani za vitu vingine ni kwamba thamani yako haipimwi kwa pesa.

Thamani yako inapimwa kwa kile unachokitoa!
Wala si kile kikuingiacho!

Kama wewe ni mtu wa kutoa matusi basi thamani yako tutaipima kwa matusi yako.

Kama wewe kila mara unabubujikwa na maneno yenye busara thamani yako tutaipima kwa busara zako.

Kama wewe hutulii ila kuhakikisha watu wanapiga hatua KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI basi thamani yako itapimwa kwa hilo.

Yaani kiufupi ni kwamba thamani yako inapimwa kwa kile unachotoa si kile unachopokea.
Aya sasa leo utatoa nini!
Utatoa nini cha thamani kubwa sana.

Ungependa watu wafaidike na nini kutoka kwako?

Ushauri Wangu;

Chagua kitu kimoja tu ambacho utatoa thamani yako hapo.
Kitu ambacho tukikiongelea hapa mjini basi jina linalokujabakilini ni jina lako..

Hivi ushawahi kujiuliza watu maarufu wanafahamika kwa vitu vingapi?

Ahaaa! Kumbe hujawahi kujiuliza hata swali hili dogo!!

Basi bwana mheshimiwa usihuzunike! Ila fahamu kwamba watu maarufu wanafahamika kwa kitu kimoja tu!

Hii ni habari ambayo sikutaka niitoe nikiwa wa kwanza ila imenilazimu kufanya hivyo.

Ngoja nikuulize, ukiulizwa kitu kimoja juu ya Diamond utasemaje?

Unafaham nini juu ya Fransis Cheka?

Kitu kimoja tu! Na hawa watu wote wanafahamika kwa kitu kimoja.

Nipo nafikiri hapa nikiulizwa kitu kimoja juu yako nitasemaje! Unanipa wakati mgumu wa Mimi kukueleza mbele ya watu.

Hivi niseme ni mpenzi wa kuchati? Au niseme ni mzembe akiyekubuu!

Niseme mvivu wa kuamka?

 Au maskini wa maarifa?

Niseme nini sasa juu yako? Kitu kimoja tu ambacho kitakutangaza ni kipi?

Bado nakitafuta sikioni.

Kachague kitu kimoja sasa ambacho utafanya.
Ili siku moja nikiulizwa basi walau na Mimi niseme kwa kujiamini kwamba ninakufahamu kwa jambo fulani.

TATIZO SI RASLIMALI ZILIZOPOTEA

tatizo ni raslimaliwatu tunazozipoteza

Wewe Ni Zaidi Ya Ulivyo.

Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI lipia sasa 5000 kwenda 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA baada ya hapo nitumie ujumbe wenye email yako. Utapokea kitabu ndani ya muda mfupi.

Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
($ongambele)
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X