Kila siku kuna watu wanajaribu fursa mpya. Endapo fursa hiyo haijafanya kazi, mtu anaachana nayo na kwenda kuchukua fursa nyingine. Isipofanya kazi unaacha. Yaani unaweza kutumia miaka Mingi sana ukijaribu huku na kuacha na kwenda kujaribu sehemu nyingine.
Binafsi huwa naipenda sana asili, maana huwa haijaribu. Bali huwa inafanya haswa.
Majani huwa hayajaribu kukua ila huwa yanakua.
Samaki huwa hajaribu kuogelea ila anaogelea.
Maua hayajaribu kuchanua ila yanachanua
Ndege hawajaribu kupaa ila wanapaa. Hii ni asili yao. Na hii ni asili ya viumbe vingine.
Viumbe hivi hata ambavyo havina akili, wala uelewa wowote vinafanya vitu haswa bila kujiwekea vikwazo.
Hakuna mti ambao unaanza kuuliza mti mwingine kama urefuke au uache. Wala hakuna mti unaoangalia pembeni kuona kama miti mingine ni mirefu na hivyo na wenyewe urefuke au uache.
Kama mti unapaswa kurefuka basi unafanya hivyo bila kuuliza wala kuangalia pembeni, kama miti mingine imerefuka au la!
Ukitaka kudhibitisha hili kapande mti wowote ambao unajua unarefuka katikati ya miti mifupi. Utarefuka tu!
Mfano mdogo ambao kila mtu anaweza kuulewa ni pale unapopanda mahindi katikati ya maharage,mahindi hayatajizuia kukua bali yatakua mpaka kufikia ukomo wake wa mwisho.
kumbe miti haijaribu kukua ila inakua
Hivi ushawahi kusikia au kuona kwamba dunia ilikuwa inajaribu kujizungusha kwenye mhimili wake?
Au hata kusikia kwamba juzi jua lilijaribu kuwaka?
Vitu hivi huwa havijaribu.
Kama dunia kujizungusha kwenye mhimili wake inazunguka kweli tena kwa sipidi kubwa. Haiogopi kwamba inaangaliwa au haiangaliwi. Vivyo hivyo ikiwa inalizunguka jua.
Sasa inakuwaje watu wanapenda kujaribu badala ya kufanya. Hii hapa ni orodha ya vitu vinavyofanya watu wajaribu.
1. Uoga
Je, watu watanionaje?
Je, nikishindwa si watanisema?
Uoga unafanya watu wengi wawe wa kujaribu jaribu. Hata pale mtu anapokutana na kikwazo cha muda ambacho kingeweza kutatuliwa basi utasikia akisema *nilikuwa najaribu
Hivi kweli wewe uko makini, au unatania. Hivi unadhani jua lingejaribu kuwaka likakuta mawingu angani lingefanyaje? Najua utasema lingeacha. Na kama lingeacha, wewe ungepata wapi mwanga. Ebu kabla ya wewe kusema kwamba nitajaribu fikiri Mara mbili, Tatu juu ya suala hilo.
Asili yetu ni kufanya si kujaribu.
Hata tukiangalia katika biblia Kitabu cha Mwanzo. Mungu hakujaribu kuumba. Bali aliumba. Kwa hiyo wewe si matokeo ya majaribio.
Sasa kama wewe si matokeo ya majaribio unajaribu ili iweje?
Badilika sasa chukua hatua.
Soma zaidi; Hutaki Kupiga Hatua
2. kupenda mafanikio ya haraka
Yaani kuna watu wanapenda afanye kitu leo kesho tayari anafurahia mafanikio makubwa.
Au kama wengi wanavyosema “mimi nataka nifanye kama fulani, maana yeye alijabu tu mishe ikatiki”
😁😁😁alijaribu na mishe ikatiki? Una uhakika? Ebu kamuulize? Utagundua amefanya kazi kwa muda mrefu sana. Amejituma asubuhi mchana na jioni. Leo hii unataka kuniambia kwamba alijaribu tu na Mishe ikatiki! Kumbuka *no research no right to speak*.
Sasa wewe mbona unajaribu jaribu. Hata kuangalizia unashindwa? Huyo mwenzako unayesema alijaribu mishe ikatiki. Unaona kwamba alifanya kitu kimoja. Sasa wewe unajaribu jaribu! Kwa nini?
Vipe vitu muda na wewe utashangazwa na matokeo makubwa utakayoyapata. Roma haikujegwa kwa siku moja. Wala ghorofa kubwa haisimimamishwi ndani ya siku moja.
Katika kuzunguka katika kona ya Biblia nikakutana na maneno yanayosema “mali iliyopatikana kwa haraka itapungua, bali yeye achumaye kidogo atazidishiwa”(Mithali 13:11)
Bonyeza hapa kujiunga na kundi langu la wasp
https://chat.whatsapp.com/C3pI1NCgaJEHaYdYW6BqVr
3. Uaminifu.
Kukosekana kwa uaminifu ndiko kunawafanya vijana wanajaribu jaribu kuhusiana.
4. kutokukubali uhalisia
Kila kitu ni matokeo. Na sisi ndio wasabibishi. Ukubali usikubali uko jinsi ulivyo kwa sababu wewe ndiwe uliyetengeneza hiyo hali ya sasa. Mimi sijui kwa sasa upokweye hali gani ila ninachojua ni kimoja tu. Wewe ndiwe uliyesababisha hiyo hali.
Je, vitu vinavyotokea kwako sasa unavipa maana gani? Je, unalalamika?
Huu ndio muda wako wa kuanza kuona ubora katika kila kitu.
Usijaribu tu ila ona ubora katika Kile kinachotokea.
Maana hata matatizo huwa si tatizo bali daraja LA kuvuka na kwenda ng’ambo.
HAKIKISHA UMEJIUMGA NA KUNDI LANGU LA WASAPU KWA KUBONYEZA LINK HAPO JUU👆🏿
Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com
#Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni