Binadamu ni watu ambao muda mwingine tunashangaza sana. Tumepewa macho mawili lakini utumiaji wa macho haya ni mdogo sana. Hii si kwa macho tu, Bali hata kwa viungo vingine. Viungo kama ubongo, pua, masikio kutaja ila vichache havijatumika haswa kama ambavyo vinastahili kuwa vimetumika.
Ukitaka kugundua hili. Mtafute rafiki yako mmoja nenda naye sehemu ambapo kuna kundi la watu (mfano kwenye chumba). Baada ya hapo mtoe nje na umuulize umeona nini?
Utashangaa hata wale waliokuwa kwenye chumba hakumbuki ni wangapi?
Utashangaa hajaona uzuri wa chumba, rangi ya chumba na mavazi waliyokuwa wamevaa watu hjayaona.
Hii ni kwa sababu tu aliishia kuangalia ila hakuona.
Je, wewe ni mmoja wapo?
Ili kupata kitabu hiki wasiliana na mimi sasa. |
Unahitaji kuwa mtu wa kuona kile kitu ambacho wengine hawaoni. Mfano Mimi nikienda sehemu, nikisiliza mazungumzo ya watu, nikiongea na watu huwa nafuatilia sana sana vitu viwili.
.
Mosi huwa nina shauku ya makala gani niandike kutokana na hiki ninachokiona?
Ni makala gani niandike kutokana na mazungmzo yangu Mimi Songambele na rafiki yangu aliye hapa mbele yangu?
Pili huwa najiuliza ni wazo gani la Biashara linaweza kutokana na kile ninachokiona. Ni kitu gani kinaweza kutokana na mazungumuzo yangu mimi Songambele na huyu rafiki aliye mbele yangu ila kikawa na manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho?
Soma zaidi; Maswali Muhimu ambayo unapaswa kujiuliza kila siku asubuhi?
Huwa napenda sana kuwa na ile hali ya kuangalia vitu kama msanii. Mchoraji anaona mchoro mzuri katika takataka zilizo pembeni mwa nyumba yako.
Mpambaji anaona pambo zuri kutoka kwenye jiwe ambao wewe unanawia miguu😄😄
Unaweza kuwa na jiwe pembeni mwa nyumba yako kwa zaidi ya miaka 10 unaliangalia tu. Ila kutokana na ukweli kwamba hujawahi kuliona ila huwa unaliangalia tu. Hivyo huoni thamani yake, wala huoni umuhimu wake. Siku moja akajitokeza mpambaji akakuomba lile jiwe. Kwa kuwa ulikuwa huoni thamani yake ukampa. Maana hata wewe ulikuwa na mpango wa kuling’oa na kulitupa. Unafurahi kwamba umepunguziwa mzigo.
Baada ya siku chache unaenda kumtembelea mchoraji au mpambaji anakuuliza unahisi hilo pambo limetokea nchi gani?
Unaanza kumwambia kitakuwa li eletwa kutika nje ya nchi!
Mara unasikia anakwambia “pambo hili limetokea pembeni mwa nyumba yako” anaendelea kusema kwamba “ni lile jiwe ulilonipa siku ile”. Anamalizia kwa kusema kwamba “sasa nilipe laki moja ili uchukue pambo hili”.
Heee! Yaani kumbe siku zote ulikuwa unanawa kwenye jiwe lenye thamani ya laki?.
Yaani jiwe lile lile ambalo nimekuwa nalipita kwa miaka zaidi ya kumi lina thamani ya laki?
Unaweza kujiuliza maswali kama hayo!
Ukakasirika kwa nini ulimpa jiwe hili.
Usikasirike! Je, unajua kwamba na wewe unalo jiwe la thamani kubwa sana ndani yako? Je, unajua kwamba jiwe hili watu waliokuzunguka hawalioni?
Kazi yangu ni kuuwasha moto. Kazi yangu ni kukuonesha jiwe hili. Ili baadae usije ukaanza kulia kwamba jiwe langu, jiwe lililokuwa pembeni mwa nyumba yangu sasa limewatajirisha watu wengine.
Nikijua hali hii inawakumba watu wengi sana. Basi nimeamua kuandaa kitabu bora sana. Ambacho kitakuonesha jiwe ambalo watu wengine hawaoni. Jiwe lenye thamani kubwa sana. Ndio ni kitabu cha kutoka SIFURI MPAKA KILELENI.
Ndani ya Kurasa za kitabu hiki utapata kujifunza na kuligundua jiwe la thamani kubwa sana lililondani yako.
Ili kupata Kitabu hiki, KUTOKA SIFURI MPAKA KILELNI. Utatuma Tsh. 5000 kwenda namba 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA.
Baada ya hapo nitumie email yako kwa namba hiyo hiyo (kupitia wasap) ili nikutumie kitabu hiki.
Kitabu hiki kipo katika mfumo wa nakala tete (soft copy) na ninakituma kwa njia ya email. Kitabu hiki kitakufikia popote pale ulipo nchini na duniani.
Kumbuka 5000 ni bei ya punguzo. Punguzo hili limeanza jana tarehe 25 mwezi wa 9 na litadumu mpaka tarehe 01 mwezi oktoba. Jipatie nakala yako sasa kwa kuwasiliana na mimi ili uweze kuligundua jiwe hili.
Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
(Songambele)
0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambele blog.blogspot.com