Fanya Kile Ambacho Wengi Wanaogopa


Habari ya siku ya leo Rafiki yangu.

Moja kati ya makosa makubwa sana ambayo waafrika tumeaminishwa na kuyakubali ni kuambiwa UKITAKA KUMFICHA KITU MWAFRIKA basi kiandike kwenye Kitabu.

Basi mimi sijui nilikuwaje maana kile ambacho watu huwa wanasema ni kigumu kufanyika hicho hicho ndicho huwa napenda nifanye kwa ubora hadi watu washangae.

Mfano nikiwa kidato cha kwanza nilikuwa nasikia vijana walionitangulia madarasa ya mbele wakisema “hesabu za kidato cha Tatu ni ngumu kuliko hesabu za o level nzima”. Katika akili yangu nilianza kutengeneza mazingira ya  kuwa mwanamahesabu mzuri nikifika kidato cha tatu. Kilichotokea baada ya Mimi kuingia kidato cha Tatu ni historia. Mpaka leo hii nikiulizwa hesabu rahisi o level nzima huwa nasema ni hesabu za kidato cha Tatu.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba sikutaka kukubali kwamba hesabu hizi ni ngumu katika akili yangu.

Sikuishia hapo tu. Kuna kipindi nikaambiwa, “dogo kama unataka kufeli kidato cha tano na cha sita kasome PCB (physics, chemistry na biology).

wqnachoogopazilivyo kwamba kile watu wanachoogopa ndicho nafanya. Niliamua kwenda kusoma PCB, kilichotokea ni historia.

Hali kama hiyo sijawahi kuiruhusu initawale katika usomanji wa vitabu. Niliposikia “ukitaka kumficha mtu kitu kakiandike kwenye Kitabu, katika akili yangu nikiwa mdogo nikaamua kwamba lazima nimiliki maktaba kubwa sana kuwahi kumilikiwa na mtu hapa duniani”.
Hata nilipokuwa shuleni tangu shule ya msingi na sekondari. Kazi kubwa ambayo nilikuwa napnda kupewa ilikuwa kazi ya kufanya kazi kwenye maktaba. Shule yetu ya msingi na sekondari ilikuwa na tabia ya kuwapa wanafunzi vitengo mbali mbali. Kwa bahati nzuri sana, sikuwahi kupewa kitengo cha maktaba hata siku moja. Ila hiyo sio kwamba iliniondolea motisha yangu ya usomaji. Mpaka leo nimeapa kwamba kama mtu ataandika kitu kwenye Kitabu kwa lengo la kunificha Mimi, basi huyo atakuwa amejidanganya. Labda ukitaka kunificha kitu kiandike facebook,instagram, au Twitter. Huko inawezekana nisikione.

Sijaandika haya yote ili kujifurahisha ila kuna somo kubwa hapa nataka uondoke nalo.

1. Hakuna mtu ambaye yupo ili kufikiri kwa niaba yako.
Kwa sababu hiyo usiwe mtu wa kusikiliza watu wengine wanasemaje. Acha watu waongee na kutoa maoni juu yako, lakini usiwasikilize. Jipe nafasi ya kufanya maamuzi mwenyewe.
Kama ningewasikiliza watu na kukubali kwamba sisi waafrika ni wazembe wa kusoma vitabu, basi leo hii nisingekuwa tayari nimeandika Kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI. unaona sasa, hasara kubwa sana ambayo ningeipata. Hasara kubwa ambayo pia wewe ungepata kwa kukosa madini adimu ambayo yameandikwa kwenye Kitabu kile na mimi.

2. Maamuzi ya maisha yako ni juu yako.
Maamuzi ya maisha unayotaka kuishi ni juu yako sisi wengine ni watazamaji. Kama unataka kuishi maisha bora, Fanya uamuzi sahihi. Laiti kama ningewasikiliza watu na kusema kwamba PCB ni ngumu. Nina hakika leo hii nisingepata nafasi ya kuwa katika chuo kikuu bora cha Kilimo hapa nchini. Lakini kwa sababu nilijua kwamba maamuzi ya maisha nayafanya mwenyewe wengine ni watazamaji basi mpaka leo hii napenda kufanya maamuzi ambayo hayapendwi na wengi ila nayapenda Mimi mwenyewe kutoka moyoni.

3. Usiogope kushindwa.
Rafiki yangu usiogope kushindwa maana watu waliofanikiwa ni wayu walioshindwa mara nyingi na hatimaye kuweza kufikia hatua kubwa sana ya kimafanikio.
Kama hujafashindwa mara nyingi sana, mafanikio yako yatakuwa ya kimashaka sana.
Ukianguka angukia mbele, nyanyuka uendelee na safari.

Ukianguka mara moja nyanyuka mara kumi.

Soma zaidi; Tatizo Si Rasilimali Zilizopotea-7

4. Chagua vizuri marafiki wako.
Moja kati ya vitu vinavyosababisha watu kushinda ni marafiki.
Na kinachosabisha watu kusindwa ni marafiki.
Kama ningesikiliza marafiki zangu wananiambia hesabu za kidato cha Tatu ni ngumu sana, basi ningetokea kuwa kilaza wa hesabu tangu kidato cha kwanza. Leo hii najiona bingwa wa hesabu hata kama sikusoma hesabu kidato cha tano na cha sita au chuo.

Wewe Ni Zaidi Ya Ulivyo Sasa,
Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.
Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA
Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com
Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  tuwasiliane kupitia 0755848391

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X