Habari Njema Kwa Watu Wote; Hawa Ndio Watu Unaowahutaji Ili Uweze Kuanza


Kila siku tumekuwa tukitaka kuanza kufanya kazi lakini tumekuwa tukiwasubiri watu kutoka maeneo mbali mbali waje ili na sisi tuweze kuendelea na kazi. Kwa bahati nzuri tumekuwa hatujui ni mtu gani na mtu gani haswa tunapaswa kumsubiria. Ndio maana tumekuwa tukisubiri kila siku na mpaka sasa ninapoandika makala haya upo sehemu umewasubiri watu waje wakwambie sasa unaweza kuanza leo.

Umesoma vitabu mbali mbali ukiwasaka watu hawa, umesikiliza audio na kuangalia video kila mahali ili upate kuwaona watu hawa.

Ila kwa siku hii ya leo mimi nimekuja na suluhisho la kila kitu. Na suluhisho hili ni hawa watu unaowahitaji na maeneo walipo. Hivyo baada ya kusoma makala haya nategemea uchukue hatua ukaongee nao watu hawa ili uweze kuanza shughuli au kazi uliyokuwa umesubiri.

Watu hawa ni
1. Wewe
2. Na wewe.

Basi, kama utawapata watu hawa inatosha wewe kuweza kufanya kazi kubwa sana.

Unajitaji wewe mwenyewe pamoja na wewe ili kazi ianze mara moja.

Kama utakuwa tayari sasa kuchukua maamuzi ya kufanya kile unachotaka usianze kusubiri sasa. Wewe fanya tu! Fanya hata kama kuna vitu havijakaa tayari, marekebisho mengine yatafanyika mbele ya safari.
Uamuzi mkubwa wa maisha ni ule unaoufanya wewe mwenyewe. Maamuzi ya mafanikio si maamuzi ya kufanyiwa na mtu mwenyewe. Ni maamuzi ya mara moja tu kwamba nitafanya kitu fulani. Inatosha. Hapa haitajiki mtu kutoka nje ya nchi kukusimamia wala haitajiki mtu kutoka Kwa Mungu wako akwambie anza.
Anayehitajika ni wewe. Na muda wa wewe kusema ninaanza ni sasa. Anza sasa.
Kama utasubiri watu milioni unaweza kuanza, hakika utasubiri sana.
Kama utasubiri watu elfumoja wakwambie anza, hakika utasubiri sana,
Kama umesubiri watu kumi wa kukwambia ndio kaka/dada sasa anzeni, hakika utasubiri sana
Kama umesubiri watu wawili wa kukwambia kwamba, kama fulani kaweza wewe umesubiri nini? Endelea kusubiri.

Watu Wawili wa kusema anza leo ni WEWE.

Ila kama umenielewa watu milioni wa kusema inawezekana ni WEWE
Watu elfu watakaokuambia ndio ni WEWE,

 Na mimi namalizia kwa kusema ni WEWE
Anza na wewe.

Soma zaidi; Ndoto Kutoka Kwa mama Yangu, Ndoto Kutoka Kwa Mwalimu Nyerere

Ulikuwa nami,
Kocha Godius Rweyongeza
Endelea kusoma makala haya ya kuelimishabna kuhamasisha kila siku.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X