Hii Ndio Biashara Ambayo Kila Mtu Anaweza Kuanzisha


Habari za siku ya leo Rafiki yangu, imani yangu kwamba jumatatu ya siku hii ya leo umeianza vyema sana na unaenda kufanya makubwa ndani ya siku hii ya leo. Kumbuka kwamba siku kama hii haitakuja kujitokeza tena.

Leo hii tunaenda kuona Biashara ambayo kila mtu anaweza kuifanya.
Makala hii imeandikwa kama jibu la swali ambalo nimeulizwa na ndugu yangu mmoja, ambaye alinitumia ujumbe huu

Habari kaka godius mm ni mwandishi WA story pia ni mwalimu lakini sijaajiliw ninao mtaji WA kiasi cha sh laki saba unanishauri nifanye biashara gani ambayo itanikwamua kimaishaaa

hata hivyo katika kuzunguka zunguka nikagundua kwamba tatizo hili ambalo linamkabili ndugu huyu si kwamba yuko peke yake ndipo nilipokutana na mwingine katika kundi langu la wasp la WHATSAP TALENT SCHOOL naye alikuwa na haya ya kusema

Japo m sio mwandishi wavitabu ila kama group member ningependa kuzungumzia hii mada
Naamin wote niayetu nikuiokoa Tanzania yetu ndo maana kaka  Edius katamugora kaandika kitabu cha barabara yamafanikio.
Ilakuna jambo ambalo linaniumiza kichwa sawa mtu unampa chachu yamafankio kwaku m inspire nakwel hyo hali inawasaidia ambao tayal wako kwenye nafasi fulani mfano uki m inspire Mwanafunz atasoma sana maana ndo jambo analofanya wakatihuo.
Ila tukiacha wanafunz tukilud kwenye maisha yakawaida kwanini tusi wa inspire watu kwakuwapa fulsa moja kwa moja.
 Kama unapompa mtu chachu yamafankio inabidi uumpe na njia yakutokea mfano bihashara ya nyanya ukifanya inakutoa au bihashara furan ukifanya kwa njia fulan utafanikiwa hyo ndo njia kuu yakumsaidia mtu kutok kwenye sehem moja  kwenda sehem nyingine. 
Maana watu wengi sana wanataman kufankiwa ila hawajui watoke kwa staili gan……………..

       

Habari, rafiki yangu.

Kuanzisha Biashara kunategemea vitu vingi sana.

1. Unapaswa kujua mazingira ulipo.
Mazingira ulipo kwa sasa yanaweza kukupa wazo zuri la biashara. Hii itategemea kama upo mjini au kijini. Biashara za kuanzisha katika mazingira haya mawili zinaweza kuwa tofauti au zikawa zilezile ila uendeshaji wa tofauti?

Swali la kujiuliza hapa, nipo mazingira gani?

2. Watu wa maeneo yale wana shida gani?
Ukiweza kutatua matatizo yanayowakabiki watu waliokuzunguka utakuwa bingwa sana na utalipwa vizuri tu.
Watu wanapenda sana kutatuliwa matatizo yao. Hivyo changamka sasa, uangalie ni vitu gani unaweza kutatua kwa kutumia matatizo ya watu waliokuzunguka.

3. Unaweza kuanzisha Biashara inayoendana na kazi unayofanya.
Umesema wewe ni mwalimu. Sijajua wewe ni mwalimu wa sekondari au shule ya msingi. Ila hiyo tayari ni fursa ya kuanzia.

Unaweza kuangalia shuleni wanafunzi wanapenda nini! Ukawafikishia huduma mapemaaa, ukaanza kuingiza chako mfukoni.

Unaweza pia kuandika vitabu vinavyoendana na mtaala wa sasa ukauza kwa wanafunzi.

Je, walimu wengine unaofanya nao kazi kitu gani wanalalamikia?
Ukiwaletea huduma wanayolalamikia utajiri utakuwa unakuita tu!

4. Kitu gani unapendelea.
Ni kitu gani ambacho unaona haiwezi kupita siku bila ya wewe kufuatilia?

Hiki ni kitu cha muhimu sana ambacho unaweza kuanza kufanya sasa. Ndugu yangu, kaa chini orodhesha vitu vya aina hii 20, sasa

Baada ya hapo nishirikishe nione umeandika vipi!!!

5. Unaweza kuanzisha Biashara juu ya kile ambacho unapenda kujifunza. Kile ambacho ungependa kupata maarifa zaidi kila siku.

Na hii ni muhimu sana. Hakikisha kwamba unachagua biashara   unayoona unapenda kujifunza. Lakini pia uwe unaipenda kwa sababu biashara huwa hazina tabia ya kusimama mara moja. Hivyo kama hutachagua Biashara yenye sifa hizi unaweza kufikia hatua ukaacha kufanya pale Biashara itakapoyumba.

6. Ungependa kusikia watu wanakuita nani?

Jina ambalo ungependa uitwe ni muhimu sana.

Je, ni kitu gani kimoja ambacho kama tutakizungumzia miaka 10,kutoka sasa, moja kwa moja uwe unahusika.
Chukulia mfano unaamua kujiusisha na Kilimo, ni zao gani ambao tukiliongelea Tanzania nzima itajja kwamba wewe hapo unaongelewa?

Chukua hatua sasa,
Wewe ni zaidi ya ulivyo

USHAURI WA ZIADA;

Kama una laki saba, usiingize yote katika biashara kwa mkupuo.

Tenga walau laki nne na nusu au laki tano, uiingize katika biashara. Laki mbili zitunze kwa ajili ya dharura zinazoweza kujitokeza njiani.

Siku zote huwa hujui kitu mpaka pale utakapokuwa umeingia ulingoni.

Hivyo vile vitu vidogo vidogo vinavyojitokeza wakati unafanya, utaweza kuvisolve kwa pesa ya ziada uliyobakiza.

Chukua hatua sasa.
Wewe Ni Zaidi Ya Ulivyo


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X