Hizi Ni Sababu Kumi Na Tatu (13) Zitakazokufanya Uingie Kwenye Kilimo Cha Bustani Leo


Habari ya siku hii ya leo Rafiki na ndugu mfuatiliaji wa makala za SONGA MBELE. Karibu sana katika makala haya ya siku hii ya leo ambapo tunakwenda kujifunza sababu saba zitakazokufanya uingie katika kikimo cha bustani siku hii ya leo.

Kwa siku sasa nimekuwa nikipokea jumbe mbali mbali kutoka kwa watu mbali mbali kutoka kona tofauti tofauti za nchi hii. Watu wamekuwa wakitaka kujua mbinu mbali mbali za Kilimo na masuala mazima yanayohusiana na  Kilimo.

Kutokana na uhitaji huo na ukizingatia mimi Godius Rweyongeza ni mtalaamu wa Kilimo katika chuo kikuu cha kilimo cha SUA nchini Tanzania. Basi nimeamua kuwa nakuletea makala moja moja juu ya Kilimo kila wiki. Makala haya yatakuwa yakikujia kila siku ya ijumaa. Ndani ya makala haya utapata kujifunza mengi juu ya Kilimo. Lakini pia nitakuunganisha na watalaamu mbali mbali wa Kilimo hapa SUA. Hivyo usikose kufuatilia mfululizo huu kila wiki.

Kilimo cha bustani ni kilimo ambacho kinazidi kupata umaarufu hapa nchini na nje ya nchi. Ni Kilimo ambacho mazao yake lazima tu yatumike kila siku. Hizi sababu saba za kwa nini uingie katika Kilimo hiki sasa.

1. Uwepo wa soko la ndani ya nchi na nje ya nchi.
Soko la mazao ya kilimo cha bustani linazidi kuongezeka kila siku. Kuna uwezekano mkubwa wa wewe kuzalisha mazao yako kijijini na ukaenda kuyauza nje ya nchi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mazao ya Kilimo cha bustani ni mazao yenye matumizi makubwa sana.

Soma zaidi; Yaboreshe mazingira yako, Fanya Zaidi

2. Uwepo wa hali nzuri ya hewa.
Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye maeneo mazuri sana yanayopata mvua kwa mwaka. Kuna maeneo ambayo yanapata mvua mara mbili kwa mwaka na maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka. Lakini bado maeneo yote yanafaa kulimwa mazao ya bustani.

3. Uwepo wa vyanzo vya maji.
Tanzania ina vyanzo vingi sana vya maji. Ambavyo. Kama sisi watanzania tutaamua kuvitumia vizuri sana tunaweza kufanya Kilimo cha umwagiliaji ambacho kinaweza kuwa kwa manufaa kwetu na kwa wengine (nje ya nchi) ambao hawana vyanzo hivi vya maji.

4. Uwepo wa ardhi ya kutosha.
Watanzania tunayo ardhi ambayo haijatumika kwa kiasi kikubwa sana. Amua sasa kuwekeza katika ardhi yako. Usisubiri waje wazungu na kuwekeza katika ardhi iliyopembeni wako ndipo uanze kulalamika, kuandamana kwamba wamechkua ardhi yetu. Amua tu kuchukua hatua maana ardhi ya watanzania ni ya kwetu. Na sisi ndio tunapewa kipaumbele katika kuwekeza.

5. Uwepo wa barabara nzuri za kusafirisha mazao ya bustani.
Kilimo cha bustani kinahusisha mazao ambayo yanaoza kwa haraka lakini pia mazao haya, ni rahisi kuharibika kama yatapigwa chini au kutopata utunzaji mzuri. Hivyo uwepo wa barabara nzuri utakusaidia  wewe kusafirisha mazao yako kwa bei nafuu. Na kusafirisha mazao yako bila kuwa na uoga kwamba yataharibika kwa sababu ya barabara.

6. Kuongezeka kwa uelewa wa watanzania juu ya utumiaji  wa mazao ya kilimo cha bustani. Kwa sasa watanzania wengi wanashauriwa na wataalamu wa afya kuhakikisha kwamba wanatumia matunda na mboga mboga. Hali hii inafanya mazao haya yanayotokana ma kilimo cha bustani kuzidi kupata soko zaidi. Chukua hatua sasa, anza kuwekeza huko.

7. Kuinuka kwa tanzania ya viwanda.
Tanzania ya viwanda inahitaji mazao ambayo mimi na wewe tunazalisha. Na asilimia kubwa ya mazao ambayo mimi na  wewe tunazalisha ni mazao ya Kilimo cha bustani. Mimi na wewe tutasimamisha na kuiwezesha Tanzania ya viwanda kwa kuhakikisha tunazo malighafi za kilimo tosha kuweza kukidhi matakwa ya soko.

8. Kuongezeka kwa wataalamu.
Kwa sasa wataalamu wanazidi kuongezeka katika kila kona ya nchi hii. Mfano wa mtaalam mzuri ni mwandishi wa ma haya. Hivyo unaweza kuwasiliana na wataalamu hawa ili wakusaidie jinsi ya kulima kilimo chenye tija.

9. Kuongezeka kwa maduka ga pembejeo.
Zamani ilikuwa vigumu kwa wakulima kuweza kuyafikia maduka ya pembejeo. Maduka haya yalikuwa katika baadhi ya miji tu hapa nchini. Lakini leo hii maduka haya yameongezeka sana. Mkulima hauhitaji utunze mbegu za msimu uliopita kwa ajili ya msimu ujao. Ila unahitaji tu kujipanga kuhakikisha unapata mbegu bora kutoka kwenye maduka ya pembejeo.

10. Uwepo wa taarifa nyingi sana kuhusu kilimo.

Kwa sasa kuna kila aina ya taarifa juu ya kilimo. Vitabu vya kilimo vipo vingi sana madukani na maeneo mengine. Lakini pia mitandao kwa sasa imejaa kila aina ya taarifa unayohitaji juu ya kilimo. Ichangamkie fursa hii.

11. Ukuaji wa teknolojia
Teknolojia ya kilimo inazidi kupanda kila siku na inazidi kuwa juu. Ikumbatie sana. Uwepo wa mashamba kitalu, na vingine vingi ni sehemu ya wewe kuanzisha biashara kubwa sana ya kilimo yenye manufaa makubwa sana.

12. Kuongezeka kwa vyombo vya usafiri katika nchi hii Kunazidi kuvuta watu wengi kuingia katika kilimo kwa maana uhakika wa kusafirisha mazao upo. Unaweza kuyasafirisha popote pale nchini kwa gharama nafuu kuliko ambavyo umewahi kutokea.

Soma zaidi; Hii Ndio Biashara Ambayo Kila Mtu Anaweza Kuifanya

13. Kuwepo kwa wazalishaji wa mimea ya kisasa (grafted plants). Aina hii ya miti kwa sasa ndio miti inayopedwa sana kupandwa na watu kwa sababu inakua kwa haraka lakini pia inatoa matunda mapema. Kama ungependa kupanda  mimea hii lakini hujui ni kwa jinsi gani unaweza kuipata. Basi wewe wasiliana na mimi nitakutumia popote pale ulipo nchini.

 Maisha ni rahisi, tukipende kilimo, kutatufanya mabilionea. Kwa leo naomba niishue hapo. Tukutane ijumaa ijayo katika makala ya kilimo kama haya.

Ulikuwa nami,
Kocha Godius Rweyongeza.
Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.
Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA
Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com
Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  tuwasiliane kupitia 0755848391

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X