Habari ya siku ya leo rafiki yangu. Leo hii ni siku bora sana ambapo tunaenda kujifunza kitu bora sana kuwahi kufundishwa hapa duniani.
Na leo tutajifunza kanuni ya 3*10. Yaani kanuni ya Tatu mara dakika kumi.
Soma Zaidi; Mambo Saba (07) Unayohutaji Kuyajua Ili Kuucheza Mchezo Wa Maisha Vizuri
Kanuni hii ndio wanayoitumia watu wengi sana ambao wanaendeleza vipaji vyao. Kanuni hii inatumiwa na wanafunzi wanaofanya vyema mashuleni. Lakini pia kanuni hii inatumiwa na watu wanaopenda kufikia mafanikio makubwa katika jambo fulani. Iko hivi, Kama unataka kuelewa kitu fulani na ili uweze kukikumbuka kwa muda mrefu, basi hupaswi kukifanya mara moja na kutulia. Kifanye tatu mara dakika kumi (3*10).
Kanuni ya Tatu mara dakika kumi inakuhitaji ufanye jambo sasa kwa dakika kumi. Utulie dakika 10 kama sehemu ya mapumuziko. Urudie tena kukifanya. Baada ya hapo utulie kwa dakika kumi. Ukimaliza kupumzika uendelee tena.
Hii ndio kusema kwamba utarudia kufanya kitu kilekile kila baada ya muda kidogo. Hii itakusaidia wewe hapo kuweza kukikumbuka kitu hiki kwa ubora wa hali ya juu sana.
Itumie kanuni hii katika kujiendeleza na kuweza kufikia hatua kubwa sana. Itumie kanuni hii kuamsha kipaji chako. Itumie kanuni hii darasani na mahali pengine pengi kadri ya kazi yako unayoifanya kwa sasa.
Soma Zaidi; NIMEZALIWA MSHINDI; Maneno Huwa
Kwa leo tunaishia hapo, imani yangu unaenda kuifanyia kazi kanuni hii.
Nakushukuru sana kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza
Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA
Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA
Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA
Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391
Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391
Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391
kila la kheri
Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391