Hivi ulishawahi kujiuliza ni kitu gani unaweza kufanya bora zaidi ya wengine?
Je, unakifahamu kitu hiki?
Kama unakifahamu kitu hiki naomba niseme hongera sana ila usiishie hapa, endelea kusoma makala hii mpaka mwisho.
Kama hukifahamu, ebu tulia kwanza usiendelee. Chukua kalamu na karatasi. Ebu jiulize swali hili. Ni kitu gani naweza kukifanya kwa ubora zaidi ya watu wengine?
Je, kipo? Andika kila kinachokuja akilini mwako.
Kama umetengeneza orodha ya vitu kumi basi chagua kimoja tu. Ambacho ungependa kujifunza zaidi na ambacho unapenda sana kuliko vyote. Fanya hicho.
Soma zaidi; Kipaji Ni Nini?
Sasa usiishie tu kusema “unajua Mimi nimegundua kile ninachoweza kufanya vizuri zaidi, nenda hatua ya ziada. Fanya zaidi, zaidi, zaidi ya wengine.
Nenda hatua ya ziada ka kile unachokifanya.
Hakikisha kila unachogusa hukiachi salama. Simaanishi uharibu, nimesema usikiache salama. Usikiache kama ukivyokikuta.
Kiongezee thamani ili kiwe cha viwango vya hali ya juu sana. Fanya zaidi ya huyo rafiki yako. Nenda hatua ya ziada.
Usisite site kufanya. Anza sasa, muda ni sasa