Je, Ni Kweli Watanzania Hawajui Kupanga


Unapanga nini?

Watu wengi sana wamekuwa wakiwalalamikia watanzania kwamba watanzania hwàjaui kupanga na kuweka malengo.
Basi baada ya kusikia hili ilinipasa nianze kufuatilia kwa umakini kuona kama ukweli nyuma ya kauli hii.

Kupata kitabu hiki wasiliana na mimi kupitia 0755848391 sasa

Swali la msingi nikilokuwa nikijiukiza je, ni kweli watanzania hawajui kupanga?

Jibu la swali hili si la moja kwa moja kama ambavyo unatarajia.

Watanzania nimegundua mipango yao mingi ipo kichwani ila haipo kwenye karatasi. Hivyo hatuwezi kuiita malengo. Hii ni kutokana na utaratibu ambao watanzania wamejiwekea kwamba wao ni wazembe wa kuandika. Hawapendi kuandika vitu na kuviweka kwenye karatasi.

Nimegndua watanzania ni wazuri kwa kupanga sherehe na mbwembwe nyingine nyingi sana za burudani ila si wepesi wa kuandika malengo juu ya maisha yao.

Soma zaidi; Hivi Ndivyo Vitu Vinavyotafutwa Kwa Wanachuo Wanaotafuta Ajira

Watanzania ni wazuri wa kupanga mitoko, utasikia wikendi hii wapi?
Ukisikia hivyo jua kwamba hapo ni suala zima la mtoko wa wikendi.

Ila watanzania wachache sana ndio wanaohusika katika kuhakikisha kwamba wanapangalia maisha yao.

Ni wachache sana ambao wanajua kwamba baada ya mwaka mmoja watakuwa wamepiga hatua gani?

Wewe upo sehemu gani?

Unajua kupanga harusi ila si maisha ya ndoa?

Au unapenda kupanga matumizi ya pesa kuliko unavyopanga kuingiza kipato?

Uko wapi?
Badilika kijana maisha yetu ni kuhakikisha kwamba tunatoka hapo tulipo na kwenda hatua ya ziada.

Anza kupanga na kuwa mtazamo chanya katika yale ambayo unayafanya sasa.

Hakikisha kwamba kila kitu kinaenda kwa mpangilio vizuri.

Usifanye  kwa sababu tu ulifanya jana.

1. Andika malengo leo hii.
Hakikisha leo haipiti.

Soma zaidi; Ujumbe Muhimu Kwa Wahitimu Wa Kidato Cha Sita

2. Penda kutimiza malengo yako kuliko unavyopenda kufanya kitu kingine.
Huwezi kuingiza pesa kama muda wako unautumia kufanya vitu ambavyo haviingizi pesa. Au vinatoa kabisa pesa mfukoni mwako.

Huwezi kufanikiwa kama unafanya vitu ambavyo vitu vya kukufelisha.

3. Panga muda wa kwenda kula hata.
Panga muda wa kwenda kula bata kila wiki ila usiende hata siku moja. Hahah! Usishangae. Ndivyo ilivyo. Akili ya binadamu inadanganyika. Fumba macho yako sasa katika sehemu ambapo hakuna makelele na usumbufu. Iambie akili yako kwamba nipo sehemu fulani nakula bata. Jione kama mtu ambaye anakula bata unazozipenda ila usithubutu kutoka nyumbani kwako kwenda kula bata.

Chukua hatua sasa.

Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.

Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA
Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com
Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  tuwasiliane kupitia 0755848391

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X