Moja kati ya vitu unavyohitaji kuwa navyo hapa duniani ni mawasiliano. Unahitaji kujifunza jinsi ya kuwasiliana na watu na kuwasilisha kile kilicho katika akili yako. Kuna watu wengi ambao ukiwaangalia mwili wao huwa unaongea kitu kikubwa sana lakini kile wanachokiwasikikisha ni kidogo na pengine wanashindwa kuwasilisha kile kilicho akilini mwao. Kumbuka kwamba ni watu wachache sana wanaoweza kusoma na kuijua lugha ya mwili hivyo utatakiwa kuongea na kuwasilisha kile kilicho moyoni mwako.
Usisubiri watu wakuonee huruma. Jifunze kuongea na kuwasilisha kile kilicho moyoni mwako. Utafiti unaonesha kwamba wanawake ndio wanaweza kuwasilisha mada kuliko wanaume. Hii ni kutokana na ile hali ya wanaume kujiona wao ni watawala na hivyo kukumbatia makosa na kuyaona kama ni sehemu ya maisha yao. Wanakumbatia udhaifu wa wao kutoweza kuwasilisha mawazo yao. Na hivyo kujiona wako sahihi katika kushindwa kwako kuwasilisha mawazo. Ila jambo la msingi unalohitaji ni wewe kujifunza kuwasiliana na kuwasilisha. Ukigundua udhaifu wako wa kuwasilisha mawazo yako, jifunze kutokana na ufhaifu huo ili uzidi kusonga mbele.
Mawasiliano mazuri yatakufanya kuwa bingwa katika kuwasilisha mawazo yako. Yatakufanya bingwa wa biashara na yatakufanya bingwa wa mahusiano.
Jifunze mawasiliano, jifunze kitu muhimu sana hapa duniani.