Moja ya swali moja ambalo nimewahi kukutana nalo ni kutoka kwa Rafiki yangu anayependa kuigiza. Aliniuliza kama ungekuwa mimi ungefanyaje?
Basi katika kuongea ilibidi nimshirikishe hatua fupi ambazo ningezifanya kwa haraka na kuanza kazi.
Zisome ili siku tukikutana usiniulize swali hili la ungekuwa mimi ungefanyaje? Badala yake utaniuliza swali jingine tofauti?
Ili Kupata kitabu hiki wasiliana na Mimi kwenye namba 0755848391 |
1. NINGEWEKA MALENGO YANGU.
Kwangu malengo ni kitu kikubwa sana ambacho ninapaswa kuwa nacho? Hata wewe ukikaa bila malengo utakuwa tu wa kuzunguka na kupeperushwa na upepo. Hivyo jambo la kwanza kabisa hakikisha kwamba unaweka malengo makubwa sasa.
Jenga picha ya jinsi unavyotaka kuwa unajiona baada ya mwaka mmoja, jenga picha ya jinsi unayotaka kujiona baada ya miaka mitano, jenga picha ya jinsi unavyotaka kujiona baada ya miaka 20. Usipokuwa na malengo basi utapeperushwa kila sehemu. Au utafuata ule usemi maarufu wa “bendera hufuata upepo”.
Kumbe hakikisha sasa, unaenda kuweka malengo. Leo isiishe bila ya wewe kuweka malengo.
Soma Zaidi; Hivi Ndivyo Unaweza Kuwanasa Watanzania Wengi Kwenye Mtego Mmoja
2. NINGEANGALIA RASLIMALI ZA KUANZIA.
Je, kuna raslimali gani za kuanzia chap chap. Ebu angalia kwenye mazingira yako sasa. Unaona kitu gani ambacho unaweza kukitumia kikakupa mwanzo wa kazi zako. Kama unapenda kuigiza kama rafiki yangu aliyeniuliza swali unaweza kuwa na simu janja ya kuanzia kurekodia video fupi fupi.
Sasa hii itakusaidia nini?
Hili litakusaidia kukupa connection zaidi. Yaani hata ikitokea paap! Unakutana na mwigizaji mwingine unaweza kumwonyesha video zako fupifupi likawa daraja la wewe kuzidi kusonga mbele. Chukua hatua sasa angalia pembeni mwako kuna nini unachoweza kuanza nacho ila kikakutoa hapo ulipo kwenda hatua ya ziada.
3. NINGEAINISHA VIKWAZO VINAVYOWEZA KUNIKWAMISHA.
Je, kuna vitu gani ambavyo unaona kama vitakurudisha nyuma katika kile utakachoanza kufanya? Unaweza ukawa hauna elimu ya kutosha. Unaweza ukawa hauna raslimali za kuanzia?
Vianishe vitu hivi kwenye karatasi yako.
Andika pia jinsi utakavyotatua vikwazo hivi.
4. NINGEANGALIA WATU WANAOWEZA KUWA MSAADA KWANGU
Je, ni watu gani ambao wanaweza kuwa msaada mkubwa kwako na kukufanya wewe uzidi kusonga mbele. Waangalie watu hawa. Wanaweza kuwa ni wazazi, walimu, mpenzi, mke au mme. Waandike wote na endelea mbele ukawaambie juu ya mpango wako huo. Waambie kwamba unategemea kitu fulani kutika kwao.
Usisite endelea mbele.
Soma Zaidi; Tembea na notebook
5. NINGEANZA SASA
Hata nisingeanza kusema, “ooh, unajua kesho ipo”? “unajua sijakaa sawa”
Hayo yote ningeyapiga chini sasa na kuanza kitu sasa. Ningeota mbali sana ila ningeanza na kidogo.
Soma Zaidi; Nianzie Wapi?
6. NINGEWEKA NIDHAMU na KAZI
Yaani ningefanya kazi kwa bidii kubwa sana. Ningefanya kazi kwa juhudi na kwa nidhamu. Ningefanya kitu kidogo kila siku. Ila mwisho wa siku najua kingeweza kunifikisha mbali.
Anza sasa
Wewe Ni Zaidi Ya Ulivyo.
One response to “Kama Ningekuwa Wewe Ningefanya Hivi?”
Nazidi kuwa nondo kila kukicha kwani mafunzo hayanjachi kapa