Kitu Kimoja Kitakachokufanya Uonekane Wa Tofauti Katika Kazi Yako


habari ya siku ya leo rafiki yangu na ndugu msomaji wa makala haya. Imani yangu sasa kwamba unazidi kubadilika na kusongambele zaidi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kile unachozidi kushibishwa hapa kila siku ni kitu ambacho kinakufanya uzidi kusogea MBELE zaidi.

Siku hii ya leo tutaangalia kitu kimoja ambacho kutakufanya wewe uonekane ni wa tofauti katika kazi zako.

Moja kati ya vitu ambavyo dunia iliyokuzunguka inajitahidi kufanya ni kuwafanya watu wote waonekane wako sawa. dunia inataka watu wote waonekane ni wa kawaida. Hata watu waliokuzunguka watajitahidi kila siku kukufanya wewe kuwa wa kawaida sana. Pale utakapowaambia juu ya ndoto zako basi hawatakubali. Wataongea maneno ya kukuangusha ili ubaki  pale pale. Sasa mimi Nina kitu kimoja tu ambacho ninaweza kukwambia. Kitu chenyewe ni kwamba kifanye unachokifanya na hakikisha unaenda hatua ya ziada.
Nenda hatua ya ziada katika kila uifanyayo. Usitake kuifanya kazi ile kwa kawaida, kama ambavyo watu wengine wanataka.

Soma zaidi ; Vitu Utakavvyojifunza Kwenye Kurasa Za Kutoka  Sifuri  Mpaka Kileleni 

Wewe nenda hatua ya ziada. Fanya zaidi ya watu wanavyotegemea ufanye.
Kama watu wanategemea usome kitabu kimoja kwa  mwezi wewe soma kumi,
Kama watu wanategemea ulime hekari moja na uipande kama wako,
Nenda hata ya ziada, panda hekari moja, ongeza na mbolea lakini pia tumia mbegu bora na za kitaalamu na hakikisha umepanda kitaalamu zaidi.

Usikubali kuwa kama ambavyo wengine wanakuwa. Usikubali kufanya kama ambavyo kila mtu anafanya. NENDA HATUA YA ZIADA.

Nenda hatua ya ziada katika masomo,
Nenda hata ya ziada katika biashara,
Nenda hatua ya ziada katikakuendeleza kipaji chako.
Wewe zaidi ya ukivyo sasa.

Soma Zaidi; Kitu Kimoja Kinachozidi Kukurudisha nyuma

Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.
Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA
Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com
Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  BONYEZA HAPA

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X